Charles Wereko-Brobby

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Charles Wereko-Brobby Ni maarufu kama Tarzan (alizaliwa 27 Machi 1953) ni mhandisi, mwanasiasa, mwanadiplomasia na mfanyabiashara nchini Ghana . Amewahi kuwa afisa mkuu mtendaji waVolta River Authority ya Ghana, wakati huo alikuwa msambazaji mkuu wa jenereta nchi. [1]

Maisha ya Awali na Elimu[hariri | hariri chanzo]

Wereko-Brobby alizaliwa Kumasi mnamo Machi 1953. Alisoma Chuo cha St. Augustine na Shule ya kifahari ya Achimota . Kisha akasoma Chuo Kikuu cha Leeds, Leeds, Uingereza ambapo alitunukiwa Shahada ya Kwanza ya Sayansi katika Uhandisi wa Mafuta na Shahada ya Uzamivu katika Uhandisi wa Nishati ya jua. Alikuwa Raisi wa Muungano wa Chuo Kikuu cha Leeds kuanzia 1978 hadi 1979, Mwafrika wa kwanza kuchaguliwa katika nafasi hiyo. [2] Wereko-Brobby pia ana Shahada ya Uzamili ya Utawala wa Biashara kutoka Chuo Kikuu cha Middlesex, Hendron, Uingereza. [2]

Maisha binafsi[hariri | hariri chanzo]

Alioa tena baada ya kuachana na Joyce Aryee, Mkurugenzi Mtendaji wa zamani wa Chamber of Mines ya Ghana na katibu wa zamani wa habari wa PNDC . Yeye pia ni mpwa wa Victor Owusu baba mwanzilishi wa NPP. [3]

Viungo Vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Ghana News Agency (31 January 2008). "I did not vacate my post - Wereko-Brobbey". Graphic Online (kwa en-gb). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-01-14. Iliwekwa mnamo 2021-01-13.  Check date values in: |date= (help)
  2. 2.0 2.1 "Dr Charles Wereko-Brobby, Biography". www.ghanaweb.com. Iliwekwa mnamo 2021-01-13. 
  3. "Victor Owusu died a pauper". www.ghanaweb.com. 31 October 2002. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-09-23. Iliwekwa mnamo 2021-01-14.  Check date values in: |date= (help)
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Charles Wereko-Brobby kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.