Chama cha Demokrasia na Maendeleo
Mandhari
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (kifupi: Chadema) ni chama cha kisiasa nchini Tanzania ambacho kuanzia mwaka 2010 kilikuwa chama kikuu cha upinzani.
Kilianzishwa tarehe 28 Mei 1992 na mwanasiasa mkongwe Edwin Mtei, aliyewahi kuwa waziri wa fedha katika miaka 1977 hadi 1979.
Mwaka 2000 chama cha Chadema hakikuwa na mgombea wa urais. Mwaka 2005 mgombea wa Chadema Freeman Mbowe alikuwa namba tatu kati ya wagombea kumi akapata asilimia 5.88 za kura.
Mwaka 2010 Chadema ilipata asilimia 27.1% na mgombea urais wa chama Wilbrod Peter Slaa na kura 4,627,923 kwa 31.75%.
Hata hivyo Chadema imekataa matokeo mengi kutokana na mchakato mzima kuwa mikononi mwa Tume ya Uchaguzi isiyo huru.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- tovuti rasmi Archived 30 Oktoba 2021 at the Wayback Machine.