Awa Thiam

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Awa Thiam

Awa Thiam (alizaliwa mnamo mwaka 1950) ni mwanasiasa, mtaalamu, mwandishi, na mwanaharakati wa Senegal.[1]. Anafanya kazi kama mkurugenzi Senegal wa Kituo cha Taifa cha msaada na mafunzo ya wanawake chini ya Wizara ya Wanawake na Watoto.[2] Zaidi ni mtetezi dhidi ya ukeketaji wa wanawake (FGM), ambapo anaongea juu yake katika kitabu chake cha 1978 (La Parole AUX Négresses).

Mwaka 1986 alitajwa kama mwanamke Mweusi aliyeweza kupaza sauti juu ya ukandamizaji na ukeketaji kwa wanawake Afrika.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kumaliza elimu ya msingi nchini Senegal, Awa Thiam alihamia Ufaransa ili kupata elimu ya juu. Wakati huo hakuwa akisoma shahada ya uzamivu katika anthropolojia ya kitamaduni tu Chuo Kikuu cha Paris VIII, lakini pia alisoma shahada ya uzamivu katika Chuo Kikuu cha Falsafa kutoka Paris I.[2].

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kathleen E. Sheldon (2005). Historical Dictionary of Women in Sub-Saharan Africa. Scarecrow Press. ISBN 978-0-8108-5331-7. 
  2. 2.0 2.1 Dior, Konate (2011). Akyeampong, Emmanuel K.; Gates, Henry Louis, wahariri. Dictionary of African Biography. Oxford University Press. ISBN 9780199857258. doi:10.1093/acref/9780195382075.001.0001. 
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Awa Thiam kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.