Anthony Anderson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Anthony Anderson
AnthonyAndersonJuly06.jpg
Anderson mnamo mwezi wa Julai, 2006
Amezaliwa Anthony Alexandre Anderson
15 Agosti 1970 (1970-08-15) (umri 41)
Los Angeles, California, U.S.
Kazi yake Mwigizaji
Miaka ya kazi 1995–mpaka sasa
Ndoa Alvina Anderson (1995-mpaka sasa)

Anthony Alexandre Anderson (amezaliwa tar. 15 Agosti, 1970) ni mwigizaji wa filamu, mchekeshaji, na mwandishi kutoka nchini Marekani. Amepata kucheza kwenye ucheshi wake mwenyewe wa All About the Andersons, vilevile kwenye igizo kama vile K-Ville, The Shield na Law & Order. Pia amepata kucheza kama mwigizaji mwandamizi kwenye filamu kama vile Transformers, The Departed, na Agent Cody Banks 2: Destination London.

Yaliyomo

[hariri] Maisha ya awali

Anderson alizaliwa mjini Los Angeles, California, akiwa kama mtoto wa Dora, mshughulikiaji simu na mwigizaji; baba yake wa kufikia, Sterling Bowman, ana miliki maduka mengi ya nguo.[1] Anderson ni mhitimu wa Los Angeles County High School for the Arts na [[Chuo Kikuu cha Howard. Amesoma na waigizaji wenzake kama vile Avery Brooks, Ruby Dee na Ossie Davis.[2]

[hariri] Shughuli

Anderson amekuwa akifanya kazi kama mwigizaji, hasa kwenye nyanja za uchekeshaji, kwa miaka mingi. Kazi zake za televisheni ni pamoja na kuonekana san akiwa kama nyota mwalikwa kwenye mfululizo wa NYPD Blue, Malcolm & Eddie, In the House, na Ally McBeal. Nyusika zake zilizokuwa zikijirudia ni pamoja na mfululizo wa Til Death na The Bernie Mac Show. Alikuwa muhusika wa kati kwenye mfululizo wa All About the Andersons, ambao uliishia kwa msimu mmoja tu kwenye televisheni ya the WB.

Miongoni mwa suhirika wake maarufu ni pamoja na filamu ya: Kangaroo Jack, My Baby's Daddy, Hustle & Flow, na Agent Cody Banks 2: Destination London.

Anderson amejiunga kwenye igizo refu la TV la uharifu la NBC, Law & Order mnamo 2008. Awali alipata kuonekana kwenye mifululizo mingine miwili ya uharifu, K-ville (akiwa kama mmoja kati ya wahusika wakuu) na The Shield.

[hariri] Kazi za uongozaji

Mnamo mwaka wa 2009, Anderson amepata kuongoza filamu-fupi ya dakika moja akishirikiana na nyota mwenzi wa kwenye Law & Order,Jeremy Sisto. Filamu hiyo ilitengenezwa kwa ajili ya Responsibility Project, mpango unganishi wa NBC na Liberty Mutual Group. Kipande hicho kilirushwa wakati wa onyesho la Law & Order katika kipengele cha "Reality Bites" mnamo tar. 16 Oktoba, 2009.

[hariri] Maisha binafsi

Mnamo mwaka wa 1995, amemwoa kipenzi chake cha roho waliokuwa wakisoma wote chuo Bi. Alvina. Wawili hao wana watoto wawili. Kwa sasa wanaishi mjini Hancock Park, Los Angeles, California.

[hariri] Filmografia

[hariri] Marejeo

[hariri] Viungo vya Nje

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine