Bawasiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Hemorrhoids
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyGeneral surgery Edit this on Wikidata
ICD-10I84.
ICD-9455
DiseasesDB10036
MedlinePlus000292
eMedicinemed/2821 emerg/242
MeSHD006484

Bawasiri (au Kikundu au Futuri au Puru au Mjiko au Hemoroidi kutoka Kiingereza hemorrhoid) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa mkundu ambayo husaidia kudhibiti kinyesi.[1][2] Katika hali yake ya fiziolojia, hutenda kazi kama mto uliotengenezwa kwa njia ya vena na tishu unganishi. Huwa patholojia ikiwa hufungana [3] kwa kuvimba au kupata inflamesheni.

Dalili za hemoroidi hulingana na mahali. Hemoroidi za ndani kwa kawaida hujitokeza kwa kinyesi kilicho na damu bila maumivu, ilhali hemoroidi za nje zinaweza kutoa dalili chache au ikiwa zina thrombasi maumivu na uvimbe katika sehemu ya mkundu. Watu wengi hurejelea kimakosa dalili yoyote inayotokea karibu na sehemu ya rektamu ya mkundu kuwa "hemoroidi" na visababishi hatari vya dalili vinapaswa kutupiliwa mbali. Huku kisababishi halisi kikisalia kutojulikana, baadhi ya vipengele vinavyoongeza shinikizo la fumbatio la ndani, hasa kufungika kwa choo, vinaaminika kuchangia ukuaji wa hemoroidi.

Matibabu ya mwanzo ya maradhi madogo hadi yale ya kawaida huwa na ongezeko la kula chakula kilicho na faiba, vinywaji ili kudumisha haidresheni, dawa za kutibu inflamesheni husaidia kwa maumivu, na mapumziko. Baadhi ya taratibu ndogo zinaweza kutekelezwa ikiwa dalili ni kali au hazistawi kwa mwelekeo wa kudhibiti usiobadilika. Upasuaji hutengewa wanaokosa kuonyesha mabadiliko. Hadi nusu ya idadi ya watu wanaweza kuwa na matatizo na hemoroidi kwa wakati fulani maishani mwao. Matokeo kwa kawaida huwa mema.

Dalili na ishara[hariri | hariri chanzo]

Hemoroidi ya nje ionekanavyo karibu na mkundu wa binadamu

Hemoroidi za ndani na za nje zinaweza kujitokeza vitofauti; hata hivyo, watu wengi wanaweza kuwa na zote mbili.[2] Kuvuja damu kunakotosha kusababisha anemia ni nadra,[4] na uvujaji wa damu unaohatarisha maisha ni nadra.[5] Watu wengi wanaweza kuona haya wanapokumbana na tatizo[4] na mara nyingi hutafuta matibabu tu wakati hali inapozidi.[2]

Za nje[hariri | hariri chanzo]

Ikiwa hazina thrombasi, hemoroidi za nje zinaweza kusababisha matatizo machache.[6] Hata hivyo, zinapokuwa na thrombasi, zinaweza kuwa na maumivu sana.[2][3] Hata hivyo, maumivu haya huisha kwa muda wa siku 2 - 3 .[4] Hata hivyo uvimbe unaweza kuchukua wiki chache kupotea.[4] kishikizo cha ngozi kinaweza kubaki baada ya kupona.[2] Ikiwa hemoroidi ni kubwa na zinasababisha madhara, zinaweza kusababisha mwasho wa ngozi iliyo karibu na pia kwa mkundu.[6]

Za ndani[hariri | hariri chanzo]

Hemoroidi za ndani kwa kawaida hujitokeza kwa uwekundu uliyo ng’aavu, bila maumivu kuvuja damu kwa rektamu wakati wa au kufuatia kusonga kwa utumbo.[2] Damu hufunika kinyesi, hali inayoitwa kinyesi kilicho na damu, huwa kwa karatasi ya chooni, au hudodoka katika bakuli ya choo.[2] Kinyesi chenyewe kwa kawaida huwa chenye rangi.[2] Dalili zingine zinaweza kuwa ni pamoja na kutoka kwa ute, kuzungukia mkundu ikiwa utashuka kupitia mkundu, mwasho, na kutoweza kuzuia kinyesi.[7][5] Hemoroidi za ndani kwa kawaida huwa na maumivu tu ikiwa zitakuwa na thrombasi au nekrotiki.[2]

Visababishi[hariri | hariri chanzo]

Kisababishi kamili cha hemoroidi hakijulikani.[8] Baadhi ya vipengele vichangiapo ni pamoja na: Mazoea ya utumbo yasiyojirudia (kufungika kwa choo au kuhara), ukosefu wa mazoezi, visababishi vya lishe (chakula kilicho na kiwango cha chini cha faiba), ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio (uchovu unaoendelea kwa muda, asitisi, ukubwa wa ndani wa fumbatio, au ujauzito), jenetiki, kutokuwepo kwa vali katika vena ya hemoroidi, na kuongezeka kwa umri.[3][4] Visababishi vingine vinayoaminiwa kuongeza hatari ni pamoja na unene, kuketi chini kwa muda mrefu,[2] kikohozi kinachoendelea kwa muda na sakafu ya pelvisi kutofanya kazi.[9] Hata hivyo, thibitisho la miungano hii, ni ya chini.

Wakati wa ujauzito, shinikizo kutoka mimba kwa fumbatio na ubadilishaji wa homoni hufanya mishipa ya hemoroidi kuwa kubwa. Kuzaa pia husabibisha ongezeko la shinikizo la ndani la fumbatio.[10] Ni nadra kwa wanawake wajawazito kuhitaji matibabu ya upasuaji, kwa sababu dalili huisha baada ya kuzaa.[3]

Pathofisiolojia[hariri | hariri chanzo]

Mito ya hemoroidi ni sehemu ya anatomi ya kawaida ya binadamu na huwa maradhi inapopitia mabadiliko yasiyo ya kawaida.[2] Kunayo mito tatu iliyo katika mfereji wa mkundu wa kawaida.[3] Hii huwa pembeni mwa kushoto, utangulizi wa kulia, na sehemu za nyuma za kulia.[4] Zimetengenezwa kwa mishipa ya damu inayoitwa sinasi, tishu unganishi na misuli nyororo bali si kwa ateri wala vena.[9] Sinasi haziwi na tishu za misuli katika kuta zao zinazotofautisha kutoka kwa vena zake.[2] Seti hii ya mishipa ya damu huitwa pleksasi ya hemoroidi.

Mito ya hemoroidi ni muhimu kwa kushikilia. Huchangia hadi asilimia 15–20% ya shinikizo la kufungika kwa mkundu wakati wa kupumzika na kukinga misuli ya spinkta ya mkundu wakati wa kupitisha kinyesi.[2] Mtu anapoketi chini, shinikizo la ndani la fumbatio huongezeka, na mito ya hemoroidi kuongezeka kwa ukubwa ikisaidia kudumisha kufungika kwa mkundu.[4] Inaaminika kuwa dalili za hemoroidi hutokea wakati miundo hii ya mishipa huteleza upande wa chini au wakati shinikizo la vena linaongezeka sana.[5] Ongezeko la spinkta ya mkundu shinikizo pia linaweza kuhusishwa katika dalili za hemoroidi.[4] Aina mbili za hemoroidi hutokea: Za ndani kutoka kwa pleksasi kubwa ya hemoroidi na za nje kutoka kwa pleksasi ndogo ya hemoroidi.[4] mstari wa denteti Hugawanya sehemu zote mbili ya hemoroidi.[4]

Utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Internal hemorrhoid grades
Grade Diagram Picture
1 Endoscopic view
2
3
4

Hemoroidi hutambuliwa kwa uchunguzi wa kimwili.[11] Uchunguzi wa kutazama mkundu na maeneo yaliyo karibu na mkundu unaweza kutambua hemoroidi za nje au zile zilizoshuka.[2] uchunguzi wa rektamu unaweza kufanywa ili kutambua uwezekano wa tyuma, ya rektamu polipsisi, prosteti iliyo kubwa, au jipu.[2] Uchunguzi huu unaweza kutofaulu bila utulizaji unaofaa kwa sababu ya maumivu ,Hata ingawa hemoroidi nyingi hazihusiani na maumivu.[3] Udhibitishaji wa kutazama kwa hemoroidi za ndani unaweza kuhitaji anoskopu, kifaa cha bomba tupu kilicho na mwanga ulioshikishwa katika mwisho wa upande mmoja .[4] Kunazo aina mbili za hemoroidi: Za nje na za ndani. Hizi zinatofautishwa na mahali zilipo kwa kuzingatia mstari wa denteti .[3] Watu wengine wanaweza kuwa na aina zote mbili za dalili kwa wakati mmoja.[4] Ikiwa maumivu yapo kuna uwezekano mkuu wa hali kuwa kupasuka kwa mkundu au hemoroidi ya nje kuliko ile ya ndani.[4]

Za ndani[hariri | hariri chanzo]

Hemoroidi za ndani ni zile ambazo huanza kutokea juu ya mstari wa denteti.[6] Huwa zimefunikwa na kolamu ya epitheliumu ambayo haina maumivu risepta inayopitisha hisia. Ziliainishwa mwaka wa 1985 katika viwango vinne kwa kuzingatia kiwango cha prolapsi.[3]

  • Kiwango I: Hakuna prolapsi. Mishipa tu ya damu inayoonekana.[11]
  • Kiwango II: Kuna prolapsi mtu anapoketi lakini inapungua yenyewe.
  • Kiwango III: Kuna prolapsi mtu anapoketi na huhitaji kupunguzwa kwa mkono.
  • Kiwango IV: Kuna prolapsi na haiwezi kupunguzwa kwa mkono.

Za nje[hariri | hariri chanzo]

Hemoroidi ya nje iliyo na thrombasi

Hemoroidi za nje Ni zile zinazotokea chini ya denteti au mstari wa pektineti.[6] Zimefunikwa kwa karibu na anodemu na kwa umbali na ngozi, zote huwa na hisia za maumivu na halijoto.

Utofautisho[hariri | hariri chanzo]

Shida nyingi za mkundu, zikiwa pamoja na kufa kwa mkundu, kupasuka kwa mkundu, jipu, saratani ya kolorekto, varisesi ya mkundu na mwasho wa mkundu huwa na dalili sawa na zinaweza kutambuliwa kimakosa kama hemoroidi.[3] Kuvuja damu kwa rektamu kunaweza pia kusababishwa na saratani ya kolorektamu, kolitisi ikiwa ni pamoja na maradhi ya inflamesheni ya utumbo, maradhi ya divetikula, na anjeodisplasia.[11] ikiwa kuna anemia, uwezekano wa visababishi vingine unapaswa kuchunguzwa.[4]

Hali nyingine zinazosababisha vidonge vya mkunduni ni pamoja na: kishikizo cha ngozi, kuchunjuka kwa mkundu, prolapsi ya rektamu, polipsi na pupila ya mkundu iliyo kubwa.[4] varisesi ya rektamu ya mkundu kwa sababu ya ongezeko la pota hipatensheni (shinikizo la damu katika mfumo wa pota ya vena) unaweza kujitokeza sawa na hemoroidi lakini ni hali tofauti.[4]

Kinga[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya vigezo vya kukinga vimependekezwa vikiwa ni pamoja na kutojikaza unapoenda haja kubwa, kuepukana na choo iliyofungika au kuhara kwa kula chakula kilicho na kiwango cha juu cha faiba na kunywa vinywaji vingi au kula nyongeza ya faiba, na kupata mazoezi ya yanayotosha.[12][4] Kutumia muda mchache ukienda haja kubwa, kutosoma ukiwa chooni ,[3] na pia kupunguza uzito kwa wale ambao wana uzito ulio mwingi zaidi na kuepukana na uinuaji wa vitu vizito.[13]

Udhibiti[hariri | hariri chanzo]

Utunzaji[hariri | hariri chanzo]

Matibabu ya kutunza huwa na lishe iliyo na faiba ya chakula, unywaji wa vinywaji ili kudumisha hidrasheni, madawa ya kuzuia inflamesheni yasiyo na steroidi (Dawa za kutibu inflamesheni), uogaji katika hali ya kuketi, na kupumzika.[3] Ongezeko la ulaji wa faiba umeonyeshwa kuboresha matokeo,[14] na hili linaweza kufanyika kwa kubadilisha chakula au kwa kula nyongeza ya faiba.[3][14] Dhibitisho la faida kutokana na uogaji katika hali ya kukaa katika wakati wowote wa matibabu hata hivyo unakosekana.[15] Ikiwa zitatumika zinapaswa kupimiwa kuwa hadi dakika 15 kwa kila wakatiI.[9]

Wakati ajenti nyingi na sapozitorisi zinapatikana kwa matibabu ya hemoroidi, kunalo dhibitisho ndogo la kudhibitisha matumizi yake.[3] Steroidi zilizo na ajenti hazipaswi kutumiwa kwa muda wa zaidi ya siku 14 zinaweza kusababisha kukonda kwa ngozi.[3] Ajenti nyingi huwa ni pamoja na mchanganyiko wa viambato hai.[9] Hivi vinaweza kuwa ni pamoja na: krimu kizuizi kama grisi au zinki oksidi, ajenti ya analijesikia kama vile lidokeni, na vasokonstrikta kama vileepinefirini.[9] Flavonoidi faida zake haziaminiki na zinaweza kudhuru.[16][9] Dalili kwa kawaida huisha kufuatia ujauzito; Kwa hivyo matibabu hucheleweshwa hadi baada ya kuzaa.[17]

Utaratibu[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya taratibu zinaweza kutekelezwa ofisini. Ingawaje kwa kawaida huwa salama, madhara hatari kama vile sepsis ya kuzunguka mkundu yanaweza kutokea kwa nadra. [11]

  • Ukanda wa mpira wa kufunga unapendekezwa kama mstari wa kwanza wa matibabu kwa wale walio na kiwango cha I hadi cha 3 cha ugonjwa.[11] Ni utaratibu ambapo mipira ya kunyumbulika huwekelewa kwa hemoroidi ya ndani angalau sentimita 1  juu ya mstari wa denteti ili kukatisha usafirishaji wa damu. Kati ya siku 5-7, hemoroidi zilizonyauka hupunguka. Ikiwa mpira umewekwa karibu sana na mstari wa denteti, maumivu makali hutokea punde tu baadaye.[3] Kiwango cha kutibu kimepatikana kuwa takribani 87%[3] na kiwango cha athari hadi 3%.[11]
  • sklerotherapia huhusisha udungaji wa anjenti ya sklerosisi, kama vile fenoli, katika hemoroidi. Hii husababisha kuporomoka kwa kuta za vena na kunyauka kwa hemoroidi. Kiwango cha ufanisi miaka minne baada ya matibabu ni ~70 %< ref name=Review09/> Ambacho kiko juu zaidi ya kile cha kutumia ukanda wa mpira wa kufunga.[11]
  • Baadhi ya njia za uunguzaji zimeonyeshanwa kuwa zinafaa kwa hemoroidi, lakini kwa kawaida hutumika tu wakati ambapo njia zingine zimefeli. Utaratibu huu unaweza kufanywa kwa kutumiaelektrokotari, mionzi ya miale isiyoonekana, upasuaji wa leza ,[3] or Upasuaji baridi.[18] Uunguzaji kwa jua inaweza kuwa suluhisho kwa ugonjwa wa kiwango cha1 au cha 2.[11] Kwa wale walio na ugonjwa wa viwango vya 3 au 4 kuna uwezekano mkubwa wa kutokea tena.[11]

Upasuaji[hariri | hariri chanzo]

Baadhi ya mbinu za upasuaji zinaweza kutumiwa ikiwa udhibiti wa utunzaji na taratibu rahisi zitafeli.[11] Matibabu yote ya upasuji huhusishwa na kiwango fulani cha athari zikiwa ni pamoja na kuvuja damu, maambukizi, msongo wa mkundu na kubakia kwa mkojo, kwa sababu ya kukaribiana kwa rektamu kwa neva zinazosafirishia kwa utumbo.[3] Kunaweza pia kuwa na hatari ndogo ya kutoweza kuzuia kinyesi, hasa kile cha kiowevu,[19][9] with rates reported between 0% and 28%.[20][9] with rates reported between 0% and 28%.[21] * Haemoroidektomi ya ukataji ni ukataji na uondoaji wa hemoroidi unaotumika tu kwa hali hatari.[3] Unahusishwa na maumivu baada ya upasuaji yanayohisika na kwa kawaida huhitaji muda wa wiki 2–4 kupona.[3] Hata hivyo, kunazo faida za muda mrefu kwa wale walio na kiwango cha tatu cha hemoroidi ikilinganishwa na ukanda wa mpira wa kufunga.[22] Ni matibabu yaliyopendekezwa kwa wale walio na hemoroidi za nje zilizotiwa thrombasi ikiwa itafanyika kati ya muda wa masaa 24-72 .[11][6] gliserali trineteti utaratibu wa lihamu ya baadaye, husaidia kwa maumivu na uponyaji.[23]

  • Yakiongozwa na-Dopla, Hemoroidi ya mkundu na ile isiyo ya uaterishaji ni matibabu madogo ya mwanzo kwa kutumia dopla ya suti iliyozidi kutambua kwa usahihi utiririkaji wa damu kwa ateri. Kisha ateri hizi ‘’hufungwa’’ na tishu iliyoshuka hurudishwa katika mahali pake pa kawaida. Ina kiwango cha juu kidogo cha kujirudia lakini inazo athari chache zikilinganishwa na hemoroidektomi. [3]
  • Upasuaji wa kutoa hemoroidi iliyofunganishwa, pia inaitwa Upasuaji wa kutoa dalili za hemoroidi iliyofunganishwa, ni utaratibu unaohusisha utolewaji wa tishu nyingi za hemoroidi zilizokuwa kubwa kwa njia isiyo ya kawaida, ukifuatwa na urudishaji wa tishu za hemoroidi zilizosalia kwenye sehemu yake ya anatomi ya kawaida. Kwa kawaida huwa na maumivu madogo na huhusishwa na kupona kwa haraka ikilinganishwa na utolewaji wa kikamilifu wa hemoroidi.[3] Hata hivyo, nafasi ya hemoroidi za kidalili kurudi ni kubwa kuliko upasuaji wa kawaida wa kutoa hemoroidi[24] na kwa hivyo inapendekezwa tu kwa kiwango cha 2 au 3 cha ugonjwa.[11]

Uenezi[hariri | hariri chanzo]

Ni vigumu kutambua kiwango cha watu wanaopata hemoroidi kwa kuwa watu wengi walio nayo huwa hawaendi kumwona mhudumu wa afya.[8][5] Hata hivyo, inaaminiwa kuwa hemoroidi za kidalili huathiri angalau asilimia 50% ya idadi ya watu katika nchi ya Marekani katika wakati fulani katika maisha yao na takribani asilimia ~5% ya idadi ya watu imeathirika kwa wakati wowote unaopeanwa.[3] Jinsia zote hupitia karibu tukio sawa la hali hii[3] Huku viwango vikieleza kati ya miaka 45 na 65 .[4] Zinapatikana sana katika Kihindi[25].[9] Matokeo ya muda mrefu kwa kawaida huwa mazuri, hata kama watu wengine wanaweza kuwa na matukio ya muda mrefu yanayojirudia.[5] Kiwango kidogo tu cha watu mwishowe huhitaji upasuaji.[9]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Kisanamu cha Kiingereza cha karne ya 11. Katika upande wa kulia ni oparesheni ya kutoa hemoroidi.

Utamkwaji wa kwanza unaojulikana wa mateso haya ni kutoka 1700 KK Misri mafunjo, ambayo ushauri: “…Hupaswi kumpa mapishi, lihamu ya ukingaji mkuu; matawi ya Akeshia, chini, yakiwa yamechanganywa na kupikwa. Paka mstari wa laini hapo -kwa na uweke katika mkundu, ili apone mara moja."[26]

Katika 460 KK, Maandishi ya kusanyo wa Hipokratiki unaeleza matibabu yaliyo sawa na ukanda wa mpira wa kufunga wa kisasa: “Na hemoroidi kwa njia sawa unaweza kuzitibu kwa kuzibadili kwa sidano na kuzifunga kwa uzi sufu ulio mnene, ili upake, na usitibu mpaka zipungue na kwa kawaida uwache moja nyuma; na mgonjwa anapopona, wacha awekwe katika njia ya Hellebore.”[26]

Maelezo ya hemoroidi pia yanapatikana kwa Biblia.[27][4]

Celsus (25 KK14 BK) alieleza ufungaji kwa uzi na taratibu za eksisheni, na kujadili uwezekano wa athari.[28] Galen alitetea kuharibika au kwa muunganisho wa ateri kwa vena, akidai kuwa ilileta upungufu wa maumivu na kuenea kwa gangrini.[28] Susruta Samhita, (Karne ya 4 – 5AD), sawa na maneno ya Hippocrates, lakini hutilia mkazo suala la usafi wa kidonda.[26] Katika karne ya 13, madaktari wa upasuaji kutoka Ulaya kama vile Lanfranc of Milan, Guy de Chauliac, Henri de Mondeville na John wa Ardene walifanya maendeleo makuu na ukuzaji wa mbinu za upasuaji.[28]

Utumizi wa kwanza wa "hemoroidi" kwa Kiingereza ulitokea mwaka wa 1398, kutoka‘’haemoroides’’ kwa Kifaransa kutoka Kilatini hæmorrhoida -ae",[29] kwa zamu kutoka Kigiriki "αἱμορροΐς" (haimorrhois), "inayoweza kutoa damu", kutoka "αἷμα" (haima), "damu"[30] + "ῥόος" (rhoos), "mtiririko",[31] kutoka kitenzi "ῥέω" (rheo), "kutiririka".[32]

Suala la kutilia maanani[hariri | hariri chanzo]

Ukumbi-wa-mchezaji maarufu wa besiboli George Brett alitolewa mchezoni katika mfululizo wa dunia1980 kwa sababu ya maumivu ya hemoroidi. Baada ya kufanyiwa upasuaji mdogo, Brettvalirudi kucheza mchezo uliofuata, akisema "...shida zangu zote ziko nyuma yangu."[33] Brett underwent further hemorrhoid surgery the following spring.[34] mtoaji maoni ya kisiasa anyeshikilia mambo Glenn Beck alifanyiwa upasuaji wa hemoroidi, baadaye akaeleza tukio alilopitia lisilopendeza katika video YouTube inayotazamwa sana ya mwaka wa 2008s.[35]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Chen, Herbert (2010). Illustrative Handbook of General Surgery. Berlin: Springer. p. 217. ISBN 1-84882-088-7. 
  2. 2.00 2.01 2.02 2.03 2.04 2.05 2.06 2.07 2.08 2.09 2.10 2.11 2.12 2.13 2.14 Schubert, MC; Sridhar, S; Schade, RR; Wexner, SD (July 2009). "What every gastroenterologist needs to know about common anorectal disorders". World J Gastroenterol 15 (26): 3201–9. ISSN 1007-9327. PMC 2710774. PMID 19598294. doi:10.3748/wjg.15.3201. 
  3. 3.00 3.01 3.02 3.03 3.04 3.05 3.06 3.07 3.08 3.09 3.10 3.11 3.12 3.13 3.14 3.15 3.16 3.17 3.18 3.19 3.20 3.21 3.22 3.23 Lorenzo-Rivero, S (August 2009). "Hemorrhoids: diagnosis and current management". Am Surg 75 (8): 635–42. PMID 19725283. 
  4. 4.00 4.01 4.02 4.03 4.04 4.05 4.06 4.07 4.08 4.09 4.10 4.11 4.12 4.13 4.14 4.15 4.16 4.17 4.18 Kaidar-Person, O; Person, B; Wexner, SD (2007 Jan). "Hemorrhoidal disease: A comprehensive review". Journal of the American College of Surgeons 204 (1): 102–17. PMID 17189119. Archived from the original on 2012-09-22. Retrieved 2013-11-28.  Unknown parameter |= ignored (help); Check date values in: |date= (help)
  5. 5.0 5.1 5.2 5.3 5.4 Davies, RJ (2006 Jun). "Haemorrhoids.". Clinical evidence (15): 711–24. PMID 16973032.  Check date values in: |date= (help)
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 Dayton, senior editor, Peter F. Lawrence; editors, Richard Bell, Merril T. (2006). Essentials of general surgery (4th ed. ed.). Philadelphia ;Baltimore: Williams & Wilkins. p. 329. ISBN 9780781750035. 
  7. Azimuddin, edited by Indru Khubchandani, Nina Paonessa, Khawaja (2009). Surgical treatment of hemorrhoids (2nd ed. ed.). New York: Springer. p. 21. ISBN 978-1-84800-313-2. 
  8. 8.0 8.1 Reese, GE; von Roon, AC; Tekkis, PP (2009 Jan 29). "Haemorrhoids.". Clinical evidence 2009. PMID 19445775.  Check date values in: |date= (help)
  9. 9.00 9.01 9.02 9.03 9.04 9.05 9.06 9.07 9.08 9.09 Beck, David (2011). The ASCRS textbook of colon and rectal surgery (2nd ed. ed.). New York: Springer. pp. 174–177. ISBN 9781441915818.  Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; name "ASCRS2011" defined multiple times with different content
  10. National Digestive Diseases Information Clearinghouse (November 2004). Hemorrhoids. Chuo cha kitaifa cha maradhi ya sukari na yale ya ummeng’enyo na figo (NIDDK), NIH. Jalada kutoka ya awali juu ya 2010-03-23. Iliwekwa mnamo 18 Machi 2010.
  11. 11.00 11.01 11.02 11.03 11.04 11.05 11.06 11.07 11.08 11.09 11.10 11.11 Rivadeneira, DE; Steele, SR; Ternent, C; Chalasani, S; Buie, WD; Rafferty, JL; Standards Practice Task Force of The American Society of Colon and Rectal, Surgeons (2011 Sep). "Practice parameters for the management of hemorrhoids (revised 2010)". Diseases of the colon and rectum 54 (9): 1059–64. PMID 21825884.  Check date values in: |date= (help)
  12. Frank J Domino (2012). The 5-Minute Clinical Consult 2013 (Griffith's 5 Minute Clinical Consult). Hagerstown, MD: Lippincott Williams & Wilkins. p. 572. ISBN 1-4511-3735-4. 
  13. Glass, [edited by] Jill C. Cash, Cheryl A. Family practice guidelines (2nd ed. ed.). New York: Springer. p. 665. ISBN 9780826118127. 
  14. 14.0 14.1 Alonso-Coello, P.; Guyatt, G. H.; Heels-Ansdell, D.; Johanson, J. F.; Lopez-Yarto, M.; Mills, E.; Zhuo, Q.; Alonso-Coello, Pablo (2005). Alonso-Coello, Pablo, ed. "Laxatives for the treatment of hemorrhoids". Cochrane Database Syst Rev (4): CD004649. PMID 16235372. doi:10.1002/14651858.CD004649.pub2. 
  15. {{cite journal|last=Lang|first=DS|coauthors=Tho, PC; Ang, EN|title=Effectiveness of the Sitz bath in managing adult patients with anorectal disorders|journal=Japan journal of nursing science : JJNS|date=2011 Dec|volume=8|issue=2|pages=115-28|pmid=22117576}}
  16. Alonso-Coello P, Zhou Q, Martinez-Zapata MJ, et al. (August 2006). "Meta-analysis of flavonoids for the treatment of haemorrhoids". Br J Surg 93 (8): 909–20. PMID 16736537. doi:10.1002/bjs.5378. 
  17. Quijano, CE; Abalos, E (2005 Jul 20). "Conservative management of symptomatic and/or complicated haemorrhoids in pregnancy and the puerperium". Cochrane database of systematic reviews (Online) (3): CD004077. PMID 16034920.  Check date values in: |date= (help)
  18. Misra, MC; Imlitemsu, (2005). "Drug treatmentof haemorrhoids". Drugs 65 (11): 1481–91. PMID 16134260. 
  19. Pescatori, M; Gagliardi, G (2008 Mar). "Postoperative complications after procedure for prolapsed hemorrhoids (PPH) and stapled transanal rectal resection (STARR) procedures". Techniques in coloproctology 12 (1): 7–19. PMID 18512007.  Check date values in: |date= (help)
  20. {{citename="Pescatori 2008">Pescatori, M; Gagliardi, G (2008 Mar). "Postoperative complications after procedure for prolapsed hemorrhoids (PPH) and stapled transanal rectal resection (STARR) procedures". Techniques in coloproctology 12 (1): 7–19. PMID 18512007.  Check date values in: |date= (help)
  21. Ommer, A; Wenger, FA; Rolfs, T; Walz, MK (2008 Nov). "Continence disorders after anal surgery--a relevant problem?". International journal of colorectal disease 23 (11): 1023–31. PMID 18629515.  Check date values in: |date= (help)
  22. Shanmugam, V; Thaha, MA; Rabindranath, KS; Campbell, KL; Steele, RJ; Loudon, MA (2005 Jul 20). "Rubber band ligation versus excisional haemorrhoidectomy for haemorrhoids". Cochrane database of systematic reviews (Online) (3): CD005034. PMID 16034963.  Check date values in: |date= (help)
  23. Ratnasingham, K; Uzzaman, M; Andreani, SM; Light, D; Patel, B (2010). "Meta-analysis of the use of glyceryl trinitrate ointment after haemorrhoidectomy as an analgesic and in promoting wound healing". International journal of surgery (London, England) 8 (8): 606–11. PMID 20691294. 
  24. Jayaraman, S; Colquhoun, PH; Malthaner, RA (2006 Oct 18). "Stapled versus conventional surgery for hemorrhoids". Cochrane database of systematic reviews (Online) (4): CD005393. PMID 17054255.  Check date values in: |date= (help)
  25. Christian Lynge, Dana; Weiss, Barry D. (2001). 20 Common Problems: Surgical Problems And Procedures In Primary Care. McGraw-Hill Professional. p. 114. ISBN 978-0-07-136002-9. 
  26. 26.0 26.1 26.2 Ellesmore, Windsor (2002). "Surgical History of Haemorrhoids". In Charles MV. Surgical Treatment of Haemorrhoids. London: Springer. 
  27. King James Bible. 1 Samuel 6 4. 
  28. 28.0 28.1 28.2 Agbo, SP (1 January 2011). "Surgical management of hemorrhoids". Journal of Surgical Technique and Case Report 3 (2): 68. doi:10.4103/2006-8808.92797. 
  29. hæmorrhoida, Charlton T. Lewis, Charles Short, A Latin Dictionary, on Perseus Digital Library
  30. αἷμα, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
  31. ῥόος, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
  32. ῥέω, Henry George Liddell, Robert Scott, A Greek-English Lexicon, on Perseus Digital Library
  33. Dick Kaegel. "Memories fill Kauffman Stadium", Major League Baseball, March 5, 2009. Retrieved on 2013-11-28. Archived from the original on 2011-06-05. 
  34. "Brett in Hospital for Surgery", The New York Times, March 1, 1981. 
  35. "Glenn Beck: Put the 'Care' Back in Health Care", Jan. 8, 2008. Retrieved on 17 September 2012. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu: