Jukumu la Soko la Hisa la Nairobi Katika Uchumi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Soko la Hisa la Nairobi hujishughulisha na ubadilishanaji wa hisa zilizosajiliwa na makampuni ya umma na Serikali pia.

Broka katika soko la hisa la Nairobi

Majukumu Kuu ya Soko la Hisa[hariri | hariri chanzo]

Hukuza utamaduni wa kuchanga[hariri | hariri chanzo]

Kununua hisa huwa mojawapo ya njia ya kuchanga pesa kwani waweza kuuza hisa zako na kupata pesa wakati wazihitaji kwa matumizi. Mfano mzuri ni wakati ambao wanafunzi hurudi shuleni, wazazi wengi huuza hisa zao ili kulipa karo ya shule za watoto wao.

Hubadilisha michango kuwa uwekezaji[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kununua hisa, hisa hizi zaweza ongezeka kwa bei hivyo basi utakapoamua kuziuza, utafaidika kifedha. Kutokana na uongezekaji wa faida ya hisa, inaweza kuchukuliwa kama njia ya uwekezaji.

Ugavi sambamba wa mali[hariri | hariri chanzo]

Soko la hisa husaidia kugawa / kueneza mali kwa makampuni yaliyoihitaji. Hii huhakikisha mali ya nchi kutumika ipasavyo badala ya kubaki kuchangwa bila kuaongezeka.

Huchangia kwa hali ya juu ya uendeshaji wa makampuni[hariri | hariri chanzo]

Hii ni kwa sababu soko la hisa huhimiza ugavi wa wenye mali kutoka kwa wanaosimamia utumizi wa mali kwa sababu sio kila wakati watu walio na mali huwa na fikira nzuri ya kibiashara na wale waliyo na fikira nzuri ya kibiashara hukosa mali wakati mwingine.

Hivyo basi, wato walio na fikira nzuri ya kibiashara waweza enda kwa soko la hisa kutafuta watu wa kufadhili biashara lake kupitia Toleo Jipya la Hisa (Kenya).

Uuzaji wa uwekezaji[hariri | hariri chanzo]

Soko la hisa huwapa wawekezaji wa makampuni mbali mbali njjia ya kuuza hisa zao.

Umuhimu wa Soko la Hisa[hariri | hariri chanzo]

Soko la hisa huwa na husaidia umma, makampuni na hata serikali kwa njia zifwatazo:

  • Usambazaji wa michango kwa uwekezaji mbali mbali yenye manufaa badala ya kuweka michango kwenye mabenki au kwa matumizi ya kila siku.
  • Ukuzi wa sekta za kifedha zinazokuza uwekezaji wa mali kama vile mabenki ya uwekezaji na makampuni ya bima.
  • Uhimizaji wa kugawanisha wenye mali kutoka kwa wanaolinda utumizi wa mali
  • Huchangia kwa hali ya juu ya uendeshaji wa makampuni hivyo basi kuchangia kwa ukuzaji wa mali
  • Husaidia makampuni kupata fedha bila kuwa na madeni
  • Uboreshaji wa njia ya kupata fedha ya kuanzisha ama kuboresha makampuni ndogo.

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]