Zhu Xi
Zhu Xi au Chu Hsi (Kichina 朱熹}}, 18 Oktoba 1130 – 23 Aprili 1200) alikuwa mwanafalsafa nchini China wakati wa Nasaba ya Song. Huhesabiwa kati ya wanafalsafa muhimi zaidi wa mwelekeo wa Ukonfusio. [1] Alikuwa mwenyeji wa jimbo la Fujian nchini China.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Zhu Xi alizaliwa huko Fujian ambako babake alikuwa mtumishi wa serikali. Alifundishwa naye hadi baba akafa wakati Zhu Xi alikuwa na umri wa miaka 13. Akaendelea na masomo yake akapita mtihani kwa watumishi wa serikali.[2] Mawazo yake mara nyingi yalipingwa akafukuzwa kazi mara kadhaa lakini aliendelea kutoa mafunzo na kuwa mashuhuri.
Zhu Xi alitunga zaidi ya vitabu 70. Akaanzisha vyuo mbalimbali na kufunza maelfu ya wanafunzi na engi wao waliendelea kuwa wataalamu mashuhuri.
Kati ya vitabu vyake "Kanuni za familia" na "Mafunzo makuu" viliendelea kuwa msingi kwa mitihani ya utumishi wa serikali ya China hadi karne ya 20.[3]