Xabi Alonso
Mandhari
Xabier "Xabi" Alonso Olano (alizaliwa 25 Novemba 1981) ni mchezaji wa zamani wa Hispania ambaye alicheza kama kiungo wa kati.
Alonso alianza kazi yake katika Real Sociedad, timu kuu ya jimbo lake la nyumbani Gipuzkoa. Baada ya muda mfupi wa mkopo huko Eibar, alichaguliwa kuwa nahodha wa timu ya Real Socieded na meneja wa wakati huo alikuwa John Toshack. Alifanikiwa katika majukumu yake, akichukua klabu yake mahali pa pili katika msimu wa 2002-03. Alihamia Liverpool mnamo Agosti 2004 kwa £ 10.5 milioni na alishinda Ligi ya Mabingwa ya UEFA msimu wake wa kwanza, chini ya meneja wa Rafael Benítez, akisawazisha bao dhidi ya Milan. Msimu uliofuata, alishinda Kombe la FA na FA Community Shield.
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Xabi Alonso kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |