Word Up!

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Word Up! lilikuwa jarida linajihusisha hasa na masuala ya vijana katika burudani na muziki kutoka nchini Marekani. Jarida hili lilikuwa sehemu ya kampuni ya Enoble Media Group.[1] Jarida lililenga sana maisha na harakati za Wamarekani Weusi katika nyanja zote ikiwa ni pamoja na vijana waimbaji, marapa, wanamitindo na kadhalika. Jarida lilikuwa linatoka mara moja kwa mwezi na lilikuwa na tabia ya kuweka mabango kibao kila kona yakiwa na hamasa kwa mashabiki wapende watu zao maarufu (walitumia usemi wa: "To Die For" celebrities). Misemo hiyo ilitamba sana katika miaka ya 1980. Sehemu kubwa ya jarida hili lilijihusisha na masuala ya muziki wa rap, Hip-hop na R&B. Makao makuu yake yalikuwa mjini Paramus, New Jersey.[1]

Mwaka wa 2006, binti wa Rev Run wa kundi la Run-D.M.C., Angela Simmons alitengeneza kachapisho kadogo chenye maandishi Word Up kilichoitwa Angela's Rundown.[2] Ilikuwa wazo la kumpa hamasa Angela atengeneze toleo lake mwenyewe la jarida kwa kufuata muundo uleule wa Word-Up! [3] Mnamo Novemba 2007 Word Up walichapisha toleo la kujitegemea la Angela[4] ambalo ndani yake alionekana rapa Bow Wow, Omarion, na yeye ANgela katika kava.

Hadi 2012, Word Up limesimama kutoa machapisho yake.[5] Toleo la mwisho lilichapishwa mwezi Aprili 2012.

Mambo madogomadogo[hariri | hariri chanzo]

Hayati The Notorious B.I.G. alitaja jarida hili katika wimbo wake wa "Juicy". Alifungua na mstari unasema: "It was all a dream, I used to read Word Up magazine". Halafu akataja picha mahususi inayonekana kwenye jarida inayoonesha Salt N Pepa wakaiwa katika limousine na Heavy D. Mstari huo pia ulipata kuonekana Jay-Z katika wimbo wake wa "Dream". Mstari huu ulitumiwa katika wimbo wa Tamar Braxton "The One".

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 "Word Up! Magazine". MondoTimes. Iliwekwa mnamo 19 December 2015.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Angela Simmons' Rundown First Issue". 
  3. "Angela Simmons gets her magazine". Rap Basement. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-02-14. Iliwekwa mnamo 2017-03-13. 
  4. "Angela Simmons Rundown Mag Debut". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-17. Iliwekwa mnamo 2017-03-13. 
  5. "Word Up! - Magazine-Agent.com". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-04-17. Iliwekwa mnamo 2017-03-13.