Nenda kwa yaliyomo

Williams Holdings

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Williams Holdings
Jina la kampuni Williams Holdings
Ilianzishwa 1982
Huduma zinazowasilishwa Uendeshaji wa kampuni zingine
Mmiliki *. Sir Nigel Rudd (Mwenyekiti)
*. Roger Carr (Mkurugenzi)
Makao Makuu ya kampuni Derby
Nchi Uingereza

Williams Holdings lilikuwa kundi kubwa la biashara la Uingereza. Lilikuwa limeorodheshwa katika Soko la Hisa la London na pia katika orodha ya FTSE 100.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kampuni hii ilianzishwa na Nigel Rudd na Brian McGowan katika eneo la Derby nchini Uingereza katika mwaka wa 1982. Lengo lao lilikuwa kununua biashara zozote zilizokuwa zikifeli. Kampuni ya kwanza ,iliyokuwa kubwa, iliyonunuliwa na Williams Holdings iliikuwa biashara ya J & HB Jackson. Biashara hii ilinunuliwa na Williams katika mwaka wa 1985. J & HB Jackson ilikuwa na makao yake katika Coventry na iliendesha biashara ya vyuma.

Williams iliendelea kunawiri na ikanunua kampuni ya Crown Berger iliyokuwa katika biashara ya rangi. Crown Berger ilinunuliwa katika mwaka wa 1987. Hapo baadaye katika mwaka wa 1988, Williams ilinunua biashara ya Pilgrim House (wamiliki wa Kidde) ya Marekani kwa bei ya £331m.Biashara ya Yale & Valor ya kufuli na gesi ilinunuliwa katika mwaka wa 1991.

Kampuni ya Williams ikaanza kuzingatia biashara za usalama katika miaka ya 1990 na ikauza biashara yake ya rangi kwa Akzo Nobel katika mwaka wa 1990. Ilipofika mwaka wa 1997, kampuni hii ilinunua kampuni ya usalama na ulinzi ya Chubb Security kwa bei ya $ milioni 2.1.

Ikabadilisha jina lake kuwa Williams plc katika mwaka wa 1998 na ikauza Kampuni ya Yale Lock Company kwa Assa Abloy katika mwaka wa 2000.

Kifo cha biashara

[hariri | hariri chanzo]

Kampuni hii iligawanyika kuwa kampuni mbili, haswa: Chubb na Kidde katika mwaka wa 2000.

  1. Nigel Rudd, My best deal Archived 2012-09-08 at Archive.today Management Today, 1 Aprili 1991
  2. Flint Group: Significant dates Archived 1 Oktoba 2010 at the Wayback Machine.
  3. Williams of Britain to buy Chubb Security New York Times, 15 Februari 1997
  4. Swedish firm to buy Williams's Yale Lock Unit Los Angeles Times, 8 Machi 2000
  5. Williams plunges 14% as margins shrink Archived 13 Januari 2011 at the Wayback Machine. Independent, 19 Julai 2000