William Wordsworth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
William Wordsworth

William Wordsworth (7 Aprili 177023 Aprili 1850) alikuwa mwandishi na mshairi muhimu wa karne ya 19 nchini Uingereza. Maandiko yake yahesabiwa kati ya fasihi ya kiromantiki na amesifiwa hasa kwa shairi ya "The Prelude" (= Utangulizi).

Maisha yake[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa kama mtoto wa mwanasheria akasoma kwenye chuo kikuu cha Cambridge. Alipokuwa mwanafunzi alipenda habari za mapinduzi ya Ufaransa akatembelea nchi hii mwaka 1890. Baadaye alichukia siasa ya mapinduzi Wafaransa walipovamia Uswisi mwaka 1798 akaendelea kusimama upande wa watetezi wa utaratibu wa kale.

Tangu 1793 alianza kutoa shairi zake zilizopendwa na wasomaji.

1805 alimwoa Mary Hutchinson akazaa naye watoto 5.

Akaendelea kuwa maarufu na mwaka 1843 akapokea cheo cha mshairi rasmi wa mfalme.

Maandiko muhimu[hariri | hariri chanzo]

  • Lyrical Ballads, with a Few Other Poems (1798)
  • Lyrical Ballads, with Other Poems (1800)
  • Poems, in Two Volumes (1807)
  • The Excursion (1814)
  • Ecclesiastical Sketches (1822)
  • The Prelude (1850, posthumous)

Marejeo ya Nje[hariri | hariri chanzo]

  • M. H. Abrams, mhariri (2000). The Norton Anthology of English Literature: Volume 2A, The Romantic Period (7th ed.). New York: W. W. Norton & Company, Inc. ISBN 0-393-97568-1. 
  • Stephen Gill, mhariri (2000). William Wordsworth: The Major Works. New York: Oxford University Press, Inc. ISBN 0-19-284044-4. 
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Viungo vingine[hariri | hariri chanzo]

Maandiko ya Wordsworth mtandaoni[hariri | hariri chanzo]