Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Nani anayeandika Wikipedia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Help:Contents

Who writes Wikipedia

Watu wanaojitolea hawa-hitaji mafunzo yoyote ya kawaida kabla ya kuanzisha makala au kuhariri makala zilizopo. Watu wanaoanzisha na kuhairiri makala katika Wikipedia wanatoka sehemu mbalimbali za dunia na wana nyanja pana za kiumri na hata kihistoria. Kila mchangiaji wa kamusi elezo hii anaitwa "Mwanawikipedia", au kikawaida zaidi huitwa "mhariri".

Wakati kundi la watu wanaofanyakazi ya kukusanya habari juu ya hoja lililotolewa, basi huzua mzozo. Kipengele cha kawaida cha Wikipedia ni uwezo wa kuwekea makala kibendera cha kuonesha unataka kufanya kipi au umefanya kipi kwenye makala - kama jinsi ilivyoelezwa kwenye ukurasa wa utatuzi wa mgongano wa kimtazamo. Kipengele hiki ni maarufu hasa kwa kutatua mizozo ya kimada, mada za kubadilisha tukio liliopo au mada nyingine zinapishana na mawazo yaliyopo. Kutatua mzozo, wahariri wenye shauku watawagawana mitazamo yao kwenye ukurasa wa majadiliano wa makala. Watajaribu kufikia muafaka kwa hivyo taswira njema zote zinaweza kuwakilishwa kwa usawa! Hii inaifanya Wikipedia kuwa si mahali pa habari tu, bali hata pa ushirikiano.

Watumiaji wengi wa Wikipedia wanashauriwa kutazama ukurasa wa historia wa makala ili kutathmini idadi ya maharirio, na taswira ya michango ya watu waliongia kwenye makala. Unaweza pia kuchungulia kwenye ukurasa wa majadiliano wa makala yoyote ilimradi upate kuona kipi wasomaji na wahariri wengine wanasemaje kuhusiana na shauri fulani.

Makala zetu nzuri zimeorodheshwa kwenye ukurasa wake. Makala za namna hiyo zimekubalika kuwa na hadhi ya "ubora" na wahariri wengine. (Ikitokea maharirio ya baadaye yakapunguza ubora wa makala iliyochaguliwa, basi mtumiaji anaweza kuiteua makala iondoshwe kwenye orodha ya makala nzuri).


Jinsi ya kuboresha makala[hariri chanzo]

Pale unapokuta makala haijaisha au haiko-sahihi, basi unaweza kuhariri makala na kuisaidia Wikipedia kutengeneza makala iliyosahihi kabisa na kufaa. Fulani anaweza kuweka kitangazo juu kabisa ya makala cha kuashiria kwamba makala inahitaji kusafishwa! Pia inawezekana kuazisha makala mpya na kuchangia habari ambazo kwenye Wikipedia bado hazipo.

Njia iliyobora ya labda kutafuta habari fulani ni afadhali ujitafutie kwa uhuru, kutafuta habari kwenye vyanzo vya kuaminika ili kuhakiki ya kwamba habari unazotafuta, kama vile vitabu, makala za jarida, habari za hadithi za televisheni, biashara na habari au tovuti. Basi hakikisha ya kwamba ni za kuaminika. Kwa miongozo zaidi juu ya kuthaminisha ubora wa makala za Wikipedia, tazama Wikipedia:Tafiti na Wikipedia. Ni sera ya Wikipedia kuandika makala za kamusi elezo ambazo ni za kuthibitika, na si kuweka habari ambazo hazina uthabiti wowote. Mtindo wa kurasa ya mwongozo wa Wikipedia ina wahamasisha wahariri kutaja vyanzo! Vyanzo vilivyotolewa maelezo vinawaruhusu wasomaji wa makala kuthitibisha kilichomo ni cha kweli.