Wikipedia:Makala ya wiki/Ulemavu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

(maelezo ya picha)

Ulemavu ni hali ya kuwa na hitilafu ya kudumu mwilini au akilini inayomzuia mtu kutekeleza shughuli zilizo kawaida katika maisha ya jamii. Unamwekea mtu mipaka asiweze kutekeleza shughuli fulani katika maisha yake, tofauti na watu wengine.

Hitilafu na ulemavu

Shirika la Afya Duniani (WHO) limeunda mfumo wa kupanga alama za ulemavu. Hapa kuna tofauti kati ya

  • hitilafu (ing. impairment) kama kukosa uwezo wa kutumia kiungo cha mwili kama kawaida
  • ulemavu (ing. disability) kama hitilafu inasababisha kukosa uwezo wa kutekeleza shughuli zinazotekelezwa na "watu wa kawaida".
  • hasara au kikwazo (ing. handicap) inayoweza kupatikana kwa mtu mwenye ulemavu akishindwa kutekeleza shughuli katika jamii.

Kwa mfano mtoto aliyeambukizwa ugonjwa wa kupooza (ing. cerebral palsy) anabaki na hitilafu ya viungo vya miguu hawezi kuvikunja wala haiwezi kubeba uzito wa mwili wake. Hitilafu hii inamzuia kutembea kwa njia ya kawaida. Kama hatibiwi hitilafu inaweza kuongezeka kwa sababu musuli ya miguu zinajikaza zaidi na zaidi. Kukosa uwezo wa kutembea ni ulemavu. Lakini kiwango chake kinaweza kupunguzwa kwa tiba na vifaa vya pekee. Akijifunza kutembea kwa kutumia vyuma vilivyofungwa kando la miguu vizuizi vya kutekeleza shughuli vinapungua sana. Kutegemeana na mazingira anapoishi ataona hasara ndogo au kubwa zaidi akitafuta njia yake katika maisha. ►Soma zaidi