Nenda kwa yaliyomo

Wikipedia:Makala ya wiki/Radi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Radi juu ya mji wa Arlington, Marekani

Radi (pia: ngurumo ya umeme) ni mwangaza na miale ya mwanga wa umeme inayotokea wakati wa ngurumo wa mvua ya radi. Katika mazungumzo ya kila siku neno radi inaweza kutaja pia sauti yenyewe na mwanga unaweza kuitwa "umeme".[1] Asili yake ni volteji inayojijenga kati ya mawingu angani yenye chaji tofauti au pia kati ya mawingu na ardhi. Volteji hii ikiongezeka mno husababisha mkondo wa umeme hewani inayoonekana kama mwangaza mkali. Mkondo unatoa pia joto kali na joti hii inasababisha kupanuka kwa hewa ghafla. Upanuzi huu unaleta sauti inayosikika kama ngurumo kama ni mbali lakini inawaza kusikika pia sawa na mshtuko wa mlipuko kama ni karibu. Kama mwendo wa radi ni kutoka mawinguni kwenda ardhi inaweza kuleta hasara kwa watu au vitu. Takriban watu 2,000 hupigwa na radi kila mwaka na mara nyingi wanakufa. Radi inayolenga ardhi huelekea kuingia sehemu ya juu mahali inapopiga. Hapa kuna mitambo ya kikingaradi ni chuma zilizopo juu ya dari ya nyumba na kuendelea hadi ndani ya ardhi kando la nyumba. ►Soma zaidi