Wikimedia Foundation

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Pitio kulingana na tarehe 10:21, 21 Novemba 2016 na Kipala (majadiliano | michango)
Nembo la Wikimedia Foundation
Wikimedia Foundation, San Francisco

Wikimedia Foundation ni shirika lisilo la kiserikali katika Marekani linaloendesha wikipedia pamoja na miradi mingine.

Shabaha yake ni usambazaji wa elimu huria inayopatikana bure kwa watu wote kwa njia ya mtandao. Ilianzishwa na Jimmy Wales mwaka 2001. Shirika linaendeleza maendeleo ya programu huria za wikiwiki zinazomruhusu msomaji si kusoma tu bali kuandika na kuhariri vilevile.

Wikimedia Foundation kama miradi yake yote si ya kibiashara na yaliyomo yote yanatungwa na wachangiaji wengi wanaojitolea bila malipo.

Mapato ya shirika hutokana na michango ya watu binafsi. Makampuni na taasisi za elimu hujitolea pia kwa kutoa kompyuta na nafasi ya kutunza data kwenye server zao.

Kati ya miradi ya Wikimedia Foundation pamoja na wikipedia kuna Wikamusi (Wiktionary), Wikiquote, Wikisource, Wikinews, Wikibooks, Wikiversity, Wikimedia Commons na Meta-Wiki.

Shirika hili haliangalii yaliyomo kama makala ya wikipedia ambayo hutungwa na jumuiya za watumiaji katika lugha zinazofikia karibu 200.

Viungo vya Nje

Makala hii kuhusu mambo ya elimu bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wikimedia Foundation kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.