Werner von Siemens

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Werner von Siemens, Picha iliyochorwa na Giacomo Brogi
Injinitreni ya umeme ya kwanza duniani kwenye maonyesho ya biashara ya Berlin 1879

Ernst Werner Siemens, tangu 1888 von Siemens, (* 13. Desemba 1816 kwenye kijiji cha Lenthe karibu na Hannover, Ujerumani; † 6 Desemba 1892 Berlin) alikuwa mvumbuzi Mjerumani, muhandisi na mwenye kampuni ya viwanda. Anajulikana kama mwanzilishaji muhimu wa teknolojia ya vifaa vya umeme.

Kampuni ya Siemens iliyoanzishwa naye bado ni moja ya makampuni makubwa ya Ujerumani na kwenye soko la kimataifa. Jina lake latumiwa kwa kipimo cha SI pitisho la umeme.

Alikuwa mtoto wa 4 wa mkulima mkubwa. Hakumaliza shule lakini alipata mafunzo ya kisayansi kwenye chuo cha jeshi la Prussia alipopanda ngazi hadi kuwa luteni. Baada ya kumaliza miaka 14 jeshini alijaribu kujipatia riziki yake kwa kubuni au kuboresha vifaa mbalimbali. Alifaulu mara ya kwanza kiuchumi alipobuni teknolojia mpya ya kupakia vijiko kwa dhahabu au fedha kwa njia ya umeme galvania.

Kati ya uvumbuzi zake za kwanza ilikuwa modeli mpya ya telegrafi iliyokuwa bora kuliko zile zilizotangulia. Kwa teknolojia hii alifaulu kupata mikataba mbalimbali ya kujenga simu za telegrafi katika nchi nyingi kama Ujerumani na Urusi. Kazi kubwa ya telegrafi ilikuwa simu kutola London hadi Kalkota (Uhindi) yenye urefu wa kilomita 11,000..

Aliendelea kubuni au kuboresha vifaa vingi akajenga injinireli ya umeme ya kwanza, mfumo wa kwanza wa taa za umeme wa kuangaza barabara (mjini Berlin), eleveta ya umeme ya kwanza na tramu ya kwanza ya umeme.

Kutokana na mafanikio yake alipewa cheo cha dokta wa heshima na 1888 Kaisari Wilhelm I wa Ujerumani alimpandisha katika cheo cha mkabaila tangu mwaka ule jina lake likawa "von" Siemens.