Walinzi wa Pwani wa Marekani
Walinzi wa Pwani wa Marekani (USCG) ni kikosi cha usalama cha baharini nchini Marekani. Ni mojawapo ya matawi sita ya kijeshi nchini Marekani. Kazi kuu ya Walinzi wa Pwani wa Marekani ni kusimamia sheria za bahari. Walinzi wa Pwani wa Marekani wana watumishi zaidi ya elfu thelathani na tano. Kunapokuwa na amani nchini, kikosi hiki kinaendeshwa chini ya Idara ya Usalama wa Taifa, lakini katika wakati wa vita kinakuwa sehemu ya Jeshi la Wanamaji la Marekani. Kikosi hiki ndicho kikosi kikubwa zaidi duniani, na ni kikubwa kuliko vikosi vya wanamaji vingi. Walinzi wa Pwani wa Marekani kilianzishwa katika mwaka wa 1790 na Katibu wa Hazina . Kilipoanzishwa kiliitiwa kikosi cha Utumishi wa Mapato ya Bahari, lakini katika mwaka wa 1915 kiliunganishwa na kikosi cha Utumishi na Ulinzi wa Bahari na kikaitwa Kikosi cha Kijeshi cha Walinzi wa Pwani wa Marekani.[1] Kikosi hiki kinaimarisha sheria katika bahari na maji chini ya mamlaka ya Marekani. Pia, kinaimarisha sheria za usalama katika pwani pa Marekani. Kama sehemu ya lengo hili, kinaamuru msaada wa usafiri wa baharini katika maji ya Marekani. Hii ni pamoja na minara ya taa, bouy’s, na violeza vya redio katika maji ya Marekani. Walinzi hawa, pia wanafuatilia viwango vya barafu katika Bahari ya Atlantiki Kaskazini mwa Bahari ya Arctic.[2] Misheni za sheria za baharini na uokoaji ni muhimu zaidi kwa kikosi hiki. Maeneo muhimu zaidi ya kupiga doria kwa kikosi hiki, ni pamoja na Ghuba ya Mexico, Ghuba ya Alaska, na sehemu za kina kifupi katika Mto Columbia, na Bahari ya Pasifiki. Pia kikosi hiki kinazuia madawa ya kulevya kuingia nchi ya Marekani na hii ni sehemu ya majukumu yake kila siku. Katika mwaka wa 2017, kikosi hiki kilizikamata dola bilioni sita za kokeini na kuwakamata watu mia saba kwa waliojaribu kuyaleta madawa ya kulevya nchini Marekani. Kila siku, kikosi hiki hukamata pauni mia nane sabini na nne za kokeini na pauni kwa tarakimu za bangi.[3] Pia, kinayaokoa maisha ya watu kumi kwa wastani kila siku.[4]
Leo, kikosi hiki kinaendesha meli za baharini mia mbili na hamsini, boti ndogo elfu mbili, na ndege mia mbili na hamsini.[5]
Walinzi wa Pwani wa Marekani kina makao makuu katika mji wa Washington D.C. kando ya Mto Anacostia. Bajeti yake katika mwaka wa 2023 ni bilioni kumi na tatu pointi themanini na mbili.[6] Kikosi hiki kina wilaya tisa kote nchini.[7]
Vifaa
[hariri | hariri chanzo]Walinzi wa Pwani wa Marekani kinaendesha meli za baharini mia mbili na hamsini. Meli hizi zimeundwa maalum kwa ajili ya bahari. Kikosi hiki kinaendesha boti ndogo elfu mbili. Boti hizi zimeundwa kufanya kazi katika maji ya upwani na maji ya bara. Boti hizi zina urefu wa chini ya futi sitini na tano. Pia, zinaendesha ndege mia mbili na hamsini kutoka besi za hewa ishirini na nne. Ndege hizi zinatumika katika misheni za umbali mrefu kama upelelezi wa bahiri na utekelezaji wa sheria dhidi ya madawa ya kulevya. Pia kinaendesha aina nyingi za helikopta.[8]
Aina za ndege za helikopta zinazoendeshwa na Kikosi cha Kijeshi cha Walinzi wa Pwani wa Marekani:
C-27 Spartan: 14 C-37A: 1 C-37B: 1 HC-130H Hercules: 14 HC-130J Hercules: 12 HC-144A Ocean Sentry: 18 MH-60 Jayhawk: 42 MH-65 Dolphin: 98[9]
Wito
[hariri | hariri chanzo]Wito wa kikosi hiki ni huu:
Kulitumikia taifa letu Kwa adhama, heshima na kujitolea kwa wajibu Tunalinda Tunakinga Tunaokoa Sisi ni Semper Paratus Sisi ni Kikosi cha Kijeshi cha Walinzi wa Pwani wa Marekani.
Alama
[hariri | hariri chanzo]Ishara wa Walinzi wa Pwani wa Marekani ni tai wa bluu na nembo ya Marekani.
Mafanikio
[hariri | hariri chanzo]Katika Vita vya Pili vya Dunia, Walinzi wa Pwani wa Marekani kilifanya doria za Bahari ya Atlantiki na kulinda kundi ya meli yilizobeba silaha dhidi ya sabmarini za Ujerumani.[10]
Katika Vitu Vya Vietnam, Walinzi wa Pwani wa Marekani walisaidia katika uokoaji . Wanamaji wengi walikufa wakati wa Vita.
Katika mwezi wa tatu mwaka wa 1989, Walinzi wa Pwani wa Marekani walisaidia kumwagika kwa mafuta ya Exxon Valdez katika Ghuba ya Alaska. Walikuwa kwenye eneo la tukia kwa miezi nne.
Walinzi wa Pwani wa Marekani walipeleka wanamaji mpaka Iraq kusaidia usalama wa bandari katika mwaka wa 1990 na 2004.
Katika mwezi wa nane mwaka wa 2005, Walinzi wa Pwani wa Marekani waliitikia kimbunga cha Katrina katika mji wa New Orleans na jimbo la Louisiana. Misheni hizi ilikuwa muhimu zaidi katika historia ya Walinzi wa Pwani wa Marekani. Watu elfu thelathini na tatu waliokelewa na wanamaji wa Walinzi wa Pwani wa Marekani.
Wanamaji Maarufu
[hariri | hariri chanzo]Frank Murkowski: Seneta wa jimbo la Alaska
G William Miller: Katibu wa Hazina wa Marekani
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "United States Coast Guard (USCG) | History & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ "United States Coast Guard (USCG) | History & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ "United States Coast Guard (USCG) | History & Facts | Britannica". www.britannica.com (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ A. B. C. News. "Inside the Coast Guard's record $6 billion year in cocaine seizures". ABC News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ "Operational_Assets". web.archive.org. 2019-10-16. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-16. Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ "USCG Budget". www.uscg.mil. Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ A. B. C. News. "Inside the Coast Guard's record $6 billion year in cocaine seizures". ABC News (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ "Operational_Assets". web.archive.org. 2019-10-16. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-16. Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ "The Coast Guard Air Fleet". Defense Media Network (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
- ↑ "USCGC Acacia (WAGL 200) (American Lighthouse Tender) - Ships hit by German U-boats during WWII - uboat.net". uboat.net. Iliwekwa mnamo 2023-04-20.
Makala bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |