Nenda kwa yaliyomo

WYSIWYG

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

WYSIWYG (unaweza kutamka wizi-wig) ni akronimu au kifupi cha Kiingereza What You See Is What You Get. Ni mfumo katika fani ya kompyuta ambako yale yanayoonyeshwa kwenye skrini yanaonekana sawa na yale yatakayotokea wakati wa kuchapisha maandishi au kwenye tovuti inayotungwa. [1]

Mwanzoni maandishi ya kiwambo yalionekana kwa herufi za namna moja tu, ilhali mtumiaji aliongeza amri kwa misimbo isiyoonekana baadaye akitaka maandishi koze, herufi kubwa au rangi tofauti. Tofauti ilifanana na yale tunayoona katika wikipedia tukibadilisha mwonekano wa "Hariri chanzo" na "Hariri" (=WYSIWYG).

Mfano wa mfumo wa misimbo

Unaandika Unapata
''italiki'' italiki

'''koza'''

koza

<big>'''Kubwa'''</big>

Kubwa

Programu za kwanza zilizosambaa mfumo wa WYZIWYG zilikuwa za Apple na Windows.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Compact Oxford English Dictionary: WYSIWYG". Oxford University Press. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-10-18. Iliwekwa mnamo 2008-08-22.