Via Campesina

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

La Vía Campesina ni shirika la kimataifa la wakulima lililoanzishwa mwaka wa 1993 huko Mons, Ubelgiji, lililoundwa na mashirika 182 katika nchi 81, [1] na kujieleza kama "vuguvugu la kimataifa ambalo linaratibu mashirika ya wakulima ya wazalishaji wadogo na wa kati, wafanyakazi wa kilimo, wanawake wa vijijini; na jamii asilia kutoka Asia, Afrika, Amerika na Ulaya".[2]

Ramani inayoonyesha nchi zilizo na wanachama wa shirika la kimataifa la wakulima, Via Campesina, kulingana na Mataifa Yanayoshiriki kama ilivyoorodheshwa orodha ya wanachama wa shirika la Via Campesina kufikia mikutano yake ya Julai 2017.

Via Campesina inatetea kilimo endelevu cha kifamilia, na ndilo kundi lililoanzisha neno "uhuru wa chakula".[3] La Vía Campesina inafanya kampeni za kutetea haki ya mkulima ya mbegu, kukomesha unyanyasaji dhidi ya wanawake, kwa mageuzi ya kilimo, na kwa ujumla kutambua haki za wakulima.[4]

  1. "Via Campesina", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-03-17, iliwekwa mnamo 2022-05-15 
  2. "Via Campesina", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-03-17, iliwekwa mnamo 2022-05-15 
  3. "Via Campesina", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-03-17, iliwekwa mnamo 2022-05-15 
  4. "Via Campesina", Wikipedia (kwa Kiingereza), 2022-03-17, iliwekwa mnamo 2022-05-15