Uwanja wa michezo wa PAM Brink

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uwanja wa michezo wa PAM Brink uwanja huu una matumizi mbalimbali na unapatikana katika maeneo ya Springs, Gauteng huko Afrika Kusini. Umefungwa kwa miaka mingi kwa sababu ya uharibifu, na uhaba wa fedha katika kuuboresha. Mara nyingi umekuwa ukitumika kwa kuchezeshea mechi za Mpira wa miguu (Soka). Ni uwanja wa nyumbani wa timu ya mpira wa miguu ya Benoni Premier United na kwa muda mrefu kimekuwa kiwanja cha timu ya Falcons, timu ya mchezo wa Ragby inayocheza katika daraja la kwanza la kombe la Currie. Uwanja huo unaweza kuhimili idadi ya watu 25,000. Ulichukua jina lake kutoka kwa P.A.M. Brink, ambaye alikuwa raisi wa shirikisho dogo la mchezo wa Ragby huko mashariki ya Transvaal kabla ya kutenguliwa na mji wa Transvaal mwaka 1947 na Meya wa mji wa Springs.


Marejeo[hariri | hariri chanzo]

[

Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa PAM Brink kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.