Uvimbe wa sikio

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Uvimbe wa sikio
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyOtolaryngology Edit this on Wikidata
ICD-10H65.-H67.
ICD-9017.40, 055.2, 381.0, 381.1, 381.2, 381.3, 381.4, 382
DiseasesDB29620 serous,
9406 suppurative
MedlinePlus000638 acute, Kigezo:MedlinePlus2 with effusion, Kigezo:MedlinePlus2 chronic
eMedicineemerg/351
ent/426 complications, ent/209 with effusion, ent/212 Medical treat., ent/211 Surgical treat. ped/1689
MeSHD010033

Uvimbe wa sikio ni kikundi cha magonjwa ya uvimbe wa sehemu ya katikati mwa sikio.[1] Aina mbili kuu ni uvimbe mkali wa sikio (AOM) na uvimbe wa sikio ulio na mchozo (OME).[2] AOM ni maambukizi yanayoanza ghafla yanayodhihirika kwa maumivu ya sikio. Katika watoto wadogo, maumivu haya yanaweza kupelekea kulia sana, na ugumu wa kulala. Decreased eating and a fever may also be present. OME is typically not associated with symptoms.[3] Mara kwa mara, mgonjwa huhisi kujaa sikioni. Ugonjwa huu hufasiliwa kama uwepo wa kiowevu kisichoambukiza cha Zaidi ya wiki mbili katika sehemu ya katikati mwa sikio kwa zaidi ya miezi mitatu. Uvimbe wa sikio wa muda mrefuunaotoa usaha (CSOM) ni uvimbe wa sehemu ya katikati mwa sikio wa zaidi ya wiki mbili unaosababisha vipindi vya kutokwa na usaha sikioni. Hali hii inaweza kuwa tatizo la uvimbe mkali wa sikio. Ni nadra usaha kuwepo.[4] Hali zote tatu zinaweza kuhusishwa na kuppoteza uwezo wa kusikia.[1][2] Kupoteza uwezo wa kusikia katika OME kunaweza kutatiza uwezo wa kusoma kwa mtoto, kwa sababu ya hali yake ya muda mrefu.[4]

Kisababishi na utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Kisababishi cha AOM kinahusiana na anatomia ya utotoni na utendakazi wa kingamwili. Bakteria au virusivinaweza kuhusishwa. Vipengele vya hatari vinahusisha: kuhatarishwa kwa moshi, utumiaji vitulizaji, na kutembelea vituo vya utunzaji. Hali hutokea mara nyingi katika watu ambao ni Wamarekani Asilia au walio na Dalili za Down.[4] OME mara nyingi hutokea kufuatia AOM lakini pia inaweza kuhusishwa na maambukizi ya sehemu ya juu ya njia ya pumzi yanayosababishwa na virusi, vitu vinavyowasha kama vile moshi, au mzio.[4][2] Kuchunguza kiwambo cha sikio ni hatua muhimu katika utambuzi sahihi.[5] Dalili za AOM ni pamoja nakuvimba au ukosefu wa mwendo wa utando wa kiwambo kutokana na kipenga cha hewa.[6][3] Mchozo mpya usiohusiana na uvimbe wa sehemu ya nje ya sikio pia ni dalili ya uwepo wa ugonjwa huu.[3]

Kinga na matibabu[hariri | hariri chanzo]

Hatua kadhaa hupunguza hataru ya uvimbe wa sehemu ya ndani ya sikio ikijumuisha: ya niumonia na chanjo ya mafua, kunyonyesha kwa maziwa ya matiti pekeekwa miezi sita ya kwanza baada ya kuzaliwa, na kuepukana na moshi wa tumbako.[3] Kwa wagonjwa walio na uvimbe wa sikio ulio na mchozo, antibiotikikwa kawaida hazisaidii kuharakisha uponyaji.[6][7] Utumiaji dawa za maumivu dhidi ya AOM ni muhimu.[3] Dawa hizi ni pamoja na: paracetamol (acetaminophen), ibuprofen, kiowevu cha kutia sikioni cha benzocaine au opioidi.[3] Katika AOM, antibiotikizinaweza kuharakishauponyaji lakin zinaweza kusababisha madhara ya baadaye.[8] Antibiotikimara nyingi hupendekezwa kwa watu walio na hali hatari ya ugonjwa auwatoto wa chini ya miaka miwili. Kwa watu walio na hali isiyo kali ya ugonjwa, antibiotiki hupendekezwa kwa watu wasiopata nafuu baada ya siku mbili au tatu.[6] Chaguo la kwanza la antibiotiki kwa kawaida huwa amoxicillin. Kwa watu wanaoambukizwa mara nyingi, kijifereji cha sikio kinaweza kupunguza uwezekano wa kurejea kwa maambukizo.[3]

Epidemiolojia[hariri | hariri chanzo]

AOM huwaadhiritakriban 11% ya watu kila mwaka kote duniani (karibu visa milioni 710 ).[9] Nusu ya visa hivi huhusisha watoto wa chini ya miaka mitano na hutokea mara nyingi katika wanaume.[4][9] Kwa watu walioathiriwa, takriban 4.8% au milioni 31 hupata uvimbe wa sikio wa muda mrefu ulio na usaha.[9] Kabla ya umri wa miaka kumi, OME huathiri takriban 80% ya watoto wakati fulani maishani.[4] Uvimbe wa sehemu ya ndani ya sikio ulisababisha vifo 2,400 mwaka wa 2013 – vilivyoshuka kutoka vifo 4,900 mwaka wa 1990.[10]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Qureishi, A; Lee, Y; Belfield, K; Birchall, JP; Daniel, M (10 January 2014). "Update on otitis media - prevention and treatment.". Infection and drug resistance 7: 15–24. PMID 24453496. doi:10.2147/IDR.S39637. 
  2. 2.0 2.1 2.2 Ear Infections (September 30, 2013). Iliwekwa mnamo 14 February 2015.
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 3.6 Lieberthal, AS; Carroll, AE; Chonmaitree, T; Ganiats, TG; Hoberman, A; Jackson, MA; Joffe, MD; Miller, DT; Rosenfeld, RM; Sevilla, XD; Schwartz, RH; Thomas, PA; Tunkel, DE (March 2013). "The diagnosis and management of acute otitis media.". Pediatrics 131 (3): e964–99. PMID 23439909. doi:10.1542/peds.2012-3488. 
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 Minovi, A; Dazert, S (2014). "Diseases of the middle ear in childhood.". GMS current topics in otorhinolaryngology, head and neck surgery 13: Doc11. PMID 25587371. doi:10.3205/cto000114. 
  5. Coker, TR; Chan, LS; Newberry, SJ; Limbos, MA; Suttorp, MJ; Shekelle, PG; Takata, GS (17 November 2010). "Diagnosis, microbial epidemiology, and antibiotic treatment of acute otitis media in children: a systematic review.". JAMA 304 (19): 2161–9. PMID 21081729. doi:10.1001/jama.2010.1651. 
  6. 6.0 6.1 6.2 Otitis Media: Physician Information Sheet (Pediatrics) (November 4, 2013). Iliwekwa mnamo 14 February 2015.
  7. van Zon, A; van der Heijden, GJ; van Dongen, TM; Burton, MJ; Schilder, AG (12 September 2012). "Antibiotics for otitis media with effusion in children.". The Cochrane database of systematic reviews 9: CD009163. PMID 22972136. doi:10.1002/14651858.CD009163.pub2. 
  8. Venekamp, RP; Sanders, S; Glasziou, PP; Del Mar, CB; Rovers, MM (31 January 2013). "Antibiotics for acute otitis media in children.". The Cochrane database of systematic reviews 1: CD000219. PMID 23440776. doi:10.1002/14651858.CD000219.pub3. 
  9. 9.0 9.1 9.2 Monasta, L; Ronfani, L; Marchetti, F; Montico, M; Vecchi Brumatti, L; Bavcar, A; Grasso, D; Barbiero, C; Tamburlini, G (2012). "Burden of disease caused by otitis media: systematic review and global estimates.". PLOS ONE 7 (4): e36226. PMC 3340347. PMID 22558393. doi:10.1371/journal.pone.0036226. 
  10. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 December 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013.". Lancet 385 (9963): 117–71. PMID 25530442. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2.