Utakaso wa kikabila

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utakaso wa kikabila ni maneno ambayo yamekuja kutumika kwa upana kuashiria aina zote za fujo zinazohusisha ukabila, kuanzia uuaji, ubakaji na mateso na hata kuhamisha wakazi kwa lazima. Kamati ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 1993 ilifafanua utakaso wa kikabila kwa ufasaha kama, "kupangwa kimakusudi kuwatoa kutoka eneo fulani, watu wa kabila fulani, kwa kutumia nguvu au kwa kuwaogofya, ili kufanya eneo hilo liwe na kabila moja tu."

Neno utakaso wa kikabila ni tofauti na neno mauaji ya kimbari. Maneno haya hayalengi maana sawa, hata hivyo utafiti wa kisomi unaonyesha kuwa maneno haya yote yanaweza kutumiwa kuelezea aina nyingi za mashambulizi dhidi ya mataifa au makabila yenye msingi wa kidini. Kwa ufupi, utakaso wa kikabila ni sawa na kuhamisha watu kutoka nchi fulani kwa lazima huku mauaji ya kimbari yakiwa sawa na "mauaji ya makusudi ya kundi fulani la kikabila, kidini au kitaifa kwa sehemu au kwa ujumla."

Kwa hiyo dhana hizo mbili ni tofauti, hata hivyo zinahusiana, "kwa maana ya kawaida na maana ya ndani, utakaso wa kikabila unasababisha mauaji ya kimbari, kwa njia ya mauaji ya halaiki ya watu yanayotendwa ili kufanya watu fulani wahame kutoka eneo fulani."

Makala hii kuhusu mambo ya sheria bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Utakaso wa kikabila kama historia yake au uhusiano wake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.