Usanifu wa kriptografia ya Java

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Njia ya usimbaji fiche hutumia ufunguo wa kidijitali ambapo huweza kuficha kilichosafirishwa na kutumwa baina ya watu wawili wanaotaka kuwasiliana na hivyo kufanya vigumu taarifa miongoni mwao kusomwa na watu wengine hususani wadukuzi.

Usanifu wa kriptografia ya Java (kifupi: JCA) ni mfumo wa kufanyia kazi na usimbaji fiche kwa kutumia lugha ya programu ya Java. Ni sehemu ya API (kiolesura cha programu) ya usalama ya Java, na ilianzishwa kwanza katika mfumo wa seti ya java ijulikanayo kama JDK 1.1 kwenye kifurushi cha usalama wa Java (java.security).

JCA hutumia usanifu kulingana na "mtengenezaji wa programu" na ina seti ya API kwa madhumuni mbalimbali, kama vile usimbaji fiche, uundaji wa ufunguo wa kidijitali maalumu kutumika katika usimbaji fiche na pia usimamizi wa ufunguo huo, uzalishaji salama wa nambari bila mpangilio, uthibitishaji wa cheti, n.k. API hizi hutoa njia rahisi kwa wasanidi kujumuisha usalama katika msimbo wa programu

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

  • Java Cryptography Extension
  • Bouncy Castle (cryptography)

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]