Nenda kwa yaliyomo

Urejelezaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alama ya kimataifa kwa urejelezaji
Kutenganisha takataka kwa ajili ya urejelezaji nchini Ujerumani (vyombo kwa karatasi, plastiki, mabaki ya chakula na mengineyo yanapaswa kutumiwa na kila nyumba; sehemu za kukusanya vyupa na nguo ziko katika mtaa)

Urejelezaji (ing. recycling) ni mbinu ya kutibu takataka ambayo wa kawaida haiwezi kutumiwa kwa shabaha ya kuokoa malighafi zilizopo ndani ya takataka na kuirejeleza kwa matumizi ya kiuchumi.

Urejelezaji unahifadhi mazingira kwa kupunguza kiasi cha sumu zinazosambaa hewani na katika maji, unapunguza gharama za vitu kwa kutunza thamani iliyobaki katika takataka.

Kwa mfano[1]

  • chupa kilichotumiwa na hata kuvunjika bado ni kioo na kioo hiki kinaweza kuyeyushwa upya kuwa kutengeneza chupa tena
  • karatasi za magazeti au vitabu zinaweza kutibiwa kuwa karatasi mpya
  • vifaa vyote vya metali kama motokaa vilivyoharibika vinaweza kutumiwa kutengeneza chuma na feleji.
  • takataka ya vyakula au majani inatibiwa kuwa mbolea mwenye thamani kwa kilimo au bustani
  • nguo zilizoharibika zinaweza kukatwa na kutumiwa kwa kutengeneza uzi mpya.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Katika historia watu waliwahi kutumia takataka na vitu vilivyochakaa tangu zamani.

  • Kwa mfano takataka ogania kama mawi ya wanyama au watu ilitumiwa kama samadi na mbolea kwenye kilimo tangu miaka mielfu.
  • matumizi ya vifaa vya metali kwa kuviyeyusha na kuunda vitu vipya yalijulikana pia.
  • karatasi mwanzoni ilitengenezwa kwa kutumia nguo zilizochakaa

Lakini mabadiliko ya maisha katika miji ya zama za viwanda na utajiri uliongezeka ulileta kutokea kwa takataka ya mchanganyiko kwa kiasi kikubwa. Mchanganyiko wa takataka ni vigumu kutenganishwa ili sehemu zake zitumiwe upya. Kwa hiyo katika jamii za zama za viwanda takataka iliongezeka kupita kiasi na suluhisho ilikuwa kuchimba mashimo makubwa au kupakiza takataka kama vilima bandia na kufunika yote kwa ardhi. Lakini baada ya muda wa miaka 20-30 ilionekana ya kwamba mikusanyiko hii ya takataka ilikuwa atari maana kiasi cha kemikali ndani yake kilongezeka: beteri ziizotupwa, kopo za rangi au vyombo vya madawa ya kusafishia nyumba na kadhalika. Katika mchakato wa kuoza kemikali ndani ya takataka hiyo zilianza mmemenyuko wa kikemia kati yao na kusababisha gesi za sumu kutokea au sumu kutirikika hadi maji chini ya ardhi na hivyo kusumisha akiba ya maji kwa umma. Hapa ilikuwa sababu moja kwa kutea kwa harakati ya kiekolojia.

Kutenganisha takataka

[hariri | hariri chanzo]

Siku hizi katika nchi zote zilizoendelea imeeleweka ya kwamba ni hatari na kuleta hasara kama takataka yote inatupwa mahali pamoja na kufunikwa tu. Inaeleweka pia ya kwamba ndani ya takataka kuna thamani kubwa ya kiuchumi. Kwa hiyo nchi nyini duniani zimeanzisha taratibu za kutengaisha takataka na kuikusanya kila aina ya takataka kwa namna ya pekee.[2]

Ilikuwa kazi ngumu ya kubadilisha kawaida za watu kuhusu takataka na nchi mbalimbali zimefanyikiwa kwa viwango tofauti. Kwa jumla nchi nyingi zinatumia mbinu ya kupandisha gharama za kukusanya takataka isiyotenganishwa (yaani kodi za manisipaa kwa kazi hii) pamoja na usimamiimkali na adhabu kwa watu wanaotupa takataka hovyo.

Katika nchi zilizoendelea kila nyumba inapaswa kuwa na ndoo za takataka zinazokusanywa na manisipaa kwa kutofautisha karatasi, takataka ogania na mengine. Katika vituo vikubwa vya kutenganisha takataka metali na plastiki zinatenganishwa, chupa kutambuliwa na kuchukuliwa na mashine na kadhalika.

Juhudi hizi zimewezesha nchi nyingi kupungaza sana kiasi cha takataka inayopaswa kutupwa na kufunikwa tu.[3] Sheria zinadai ya kwamba takataka zenye kemikali (kama rangi, mabaki ya madawa) inapaswa kukusanywa pekee kwa shabaha ya kuiharibu kabisa katika majiko ya joto kali nila kutoa sumu kwenye mazingira.

  1. Common Recyclable Materials
  2. "The Best Recycling Programs in the US & Around The World". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-05-12. Iliwekwa mnamo 2015-05-24.
  3. The truth abot recycling (The Economist Jun 7th 2007)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu mambo ya teknolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hiyo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.