Uranometria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uranometria ni kitabu cha ramani ya nyota kilichotolewa mnamo mwaka 1603 na mwanaastronomia Mjerumani Johann Bayer. Kwa jumla kulikuwa na ramani 51 zilizoonyesha makundinyota yote yaliyojulikana wakati ule pamoja na makundinyota 12 ya angakusi yaliyobuniwa na Pieter Dirkszoon Keyser.

Kitabu hiki kilikuwa muhimu kwa kusambaza mfumo wa majina ya nyota uliobuniwa na Bayer na kutumiwa hadi leo kama Majina ya Bayer (Bayer designation).

Marejeo ya Nje

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Astrowiki.PNG
Mradi wa Astronomia Makala hii imewahi kukaguliwa na kuboreshwa kwenye warsha ya pamoja ya Jenga Wikipedia ya Kiswahili, Wikimedia Community User Group Tanzania na ASSAT. Imepewa hali ya ulinzi. Tunaomba mapendekezo yote ya usahihisho na nyongeza zipelekwe kwanza kwenye ukurasa wa majadiliano