Nenda kwa yaliyomo

Ulaanbaatar

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ulaanbaatar
Barabarani Ulaanbaatar

Ulaanbaatar (pia: Ulan Bator; Kimongolia Улаанбаатар - "mshujaa mwekundu") ni mji mkuu wa Mongolia mwenye wakazi 844,818. Sehemu ya wakazi hufuata mapokeo ya Mongolia wakiishi mjini miezi ya baridi tu lakini miezi ya joto huhamahama kwenye hema pamoja na mifugo yao.

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]
Hali ya Hewa ya Ulanbaatar

Mji uko kwenye nyanda za juu kwa kimo cha m 1352 kando la mto Tuul na mlima Bogd Khan Uul. Karibu nusu ya wakazi wote wa Mongolia wanaishi hapa. Takriban theluthi ya watu wa Ulanbaatar wanaishi katika hema za yurt (nyumba za kijadi) wanapochoma makaa wakati wa baridi na halii hii inaogeza sana machafuko wa hewa. Machafuko wa hewa katika miezi ya bbadiri ni tatizo kubwa wa jiji hili.

Hali ya hewa

[hariri | hariri chanzo]

Ulanbaatar imeitwa mji mkuu baridi duniani mwenye -2 °C kwa wastani ya halijoto ya mwaka. Sababu yake ni baridi kali katika miezi ya Novemba hadi Machi (mchana -10 bis -15 °C, usiku -25 °C). Wakati wa Juni hadi Agosti kuna joto kiasi (mchana 20 °C, usiku 10 °C).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji ulianzishwa kama makao ya mkuu wa wamonaki wa Kibuddha katika Mongolia. Awali makao haya yalihamahama lakini tangu 1778 uko mahali ulipo. Majina yalibadilika. Tangu 1924 serikali ya kikomunisti ilianzisha jina la Ulaanbaatar.

Kabla ya mapinduzi ya kikomunisti ilikuwa makao makuu ya kiongozi wa kidini pia ya kisiasa ya Wamongolia. Mjui ulikua tangu 1860 kama kituo cha biashara ya chai kati ya China na Urusi.

Kati ya 1904 na 1908 kiongozi wa Tibet Dalai Lama alihamia hapo kwa kuwakimbia Waingereza waliokuwa waliingia Tibet wakati ule.

Baada ya kuporomoka ya milki ya China mwaka 1911 na Mongolia kutafuta uhuru wake mji ukawa mji mkuu wa nchi mpya chini ya uongozi wa Wakomunisti waliosaidiwa na Urusi.

Sehemu kubwa ya Ulanbaatar ilijengwa wakati wa utawala wa kikomunisti kwa kuiga mfano wa miji ya Urusi.

Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]

[Booming Ulan Bator, the world's coldest capital, is choking on smoke (Los Angeles Times 16 Mei 2015)

Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ulaanbaatar kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: