Ukuta wa China

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukuta mkubwa wa China
Mstari nyekundu unaonyesha mahali pa ukuta mkubwa wa China.

Ukuta mkubwa wa China ni kati ya majengo makubwa kabisa yaliyowahi kujengwa duniani. Ni mfululizo wa kuta na ngome unaofuata mpaka kati ya China na mbuga baridi za Asia ya Kaskazini na Asia ya Kati. Ulijengwa kwa shabaha ya kulinda China dhidi ya mashambulio ya makabila ya wahamiaji wa sehemu hizo.

Jumla ya kuta zote ina urefu wa kilomita zaidi ya 21,000. [1][2]

Ujenzi ulianza katika karne ya 7 KK na kuendelea hadi karne ya 16 BK.[3]

Historia ya ukuta[hariri | hariri chanzo]

Ukuta ulijengwa na nasaba mbalimbali za watawala wa China tangu mwaka 200 KK. Shabaha yake ilikuwa ulinzi wa milki dhidi ya mataifa na makabila wa kaskazini walioendelea kushambulia China. Watu wa kaskazini walikuwa wahamiaji waliotumia farasi na ngamia, hivyo haikuwa rahisi kujua ni wapi watakapojaribu kuingia.

Ukuta jinsi ulivyo ni ukuta wa nasaba ya Ming uliojengwa kuanzia mnamo mwaka 1500. Mnamo mwaka 1700 ukuta uliachwa bila kutunzwa tena kwa sababu katika karne ya 17 sehemu kubwa za Mongolia nje ya ukuta ziliunganishwa na China.

Vipimo[hariri | hariri chanzo]

Sehemu ya ukuta iliyotengenezwa upya na kutembelewa na watalii

Ukuta huwa na upana kati ya mita 4 hadi 8 na kimo cha mita 6 hadi 9.

Kila baada ya mita mia minara ilijengwa ukutani. Minara hii ilikuwa vituo vya kulala kwa walinzi, pia ngome zao wakati wa kushambuliwa na vituo vya mawasiliano kati ya mnara na mnara. Kwa jumla ukuta ulikuwa na minara 25,000.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. China's Great Wall is 21,196 km long: survey (tovuti ya habari ya xinhua 5 Juni 2012, ikiangaliwa tar. 2 Novemba 2016)
  2. Great Wall much longer than previously believed: survey, tovuti ya gazeti la Chinadaily ya terehe 13 Juni 2012, ikiangaliwa 2 Novemba 2016
  3. Great Wall of China, Encycloüpedia Britannica online, ikiangaliwa 2.11. 2016

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ukuta wa China kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.