Nenda kwa yaliyomo

Ujarabati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ujarabati ni nadharia ya ujuzi inayozingatia tu mambo halisi yanayohisika kwa fikira na mishipa ya fahamu ya mtu. Kwa watetezi wa nadharia hii, ujuzi hupatika kwa hisi na ufahamu. Bayana ya namna hii huitwa bayana jarabati. Ujarabati ni msimamo mmojawapo katika nadharia za ujuzi, mingineyo mikuu ikiwa umantiki na ushuku.[1]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Wafula, Richard (2022). "Itikadi na Ufundishaji wa Nadharia za Uhakiki wa Fasihi". Kioo cha Lugha. 20 (1): 55–56. doi:10.4314/kcl.v20i1.4.