Uhuru Gardens
Mandhari
Uhuru Gardens ni eneo la burudani lililoko karibu na Wilson Airport, barabara ya Langata. Bustani hii ni kumbukumbu kubwa zaidi mjini Nairobi ya vita vya uhuru nchini Kenya. Sanamu ya Uhuru limejengwa pahali Uhuru kutoka kwa uingereza ulitangazwa saa sita usiku tarehe 12 Desemba 1963. Sanamu hii ina urefu wa mita 24 na hushikilia jozi la mikono iliyoshikana na njiwa wa amani. Sanamu hii iko juu ya sanamu ya wapiganiaji uhuru wakipandisha uhuru. Bustani hii iko na chemichemi ya muziki na jukwaa la kuangalilia.
Mwaka 2003, bustani hii ilikuwa pahali pa kuharibiwa kwa silaha haramu. Sherehe hii ilifanyika katika kumbukumbu ya tatu ya tamko la silaha ndogo na silaha nyepesi.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Uhuru Gardens Ilihifadhiwa 15 Machi 2010 kwenye Wayback Machine.