Ugonjwa wa asubuhi
Ugonjwa wa asubuhi (kwa lugha ya Kiingereza: morning sickness; pia hujulikana kama emesis gravidarum, kichefuchefu cha wajawazito, kichefuchefu, kutapika kwa mimba au ugonjwa wa mimba) ni hali ambayo huathiri zaidi ya nusu ya wanawake wajawazito, na vilevile baadhi ya wanawake ambao hutumia homoni za uzazi wa mpango au tiba ya kurekebisha homoni. Kwa kawaida, humshika mwanamke mjamzito mapema asubuhi na hupungua siku ikiendelea.
Kichefuchefu kinaweza kuwa halisi kali au kutapika. Katika kesi zilizokithiri, kutapika kunaweza kuwa kali na ugonjwa huu unaweza kusababisha kupungua kwa maji mwilini, kupoteza uzito, alkalosis na hypokalemia. Hali hii ilyokithiri inajulikana kama hyperemesis gravidarum na hutokea katika asilimia 1 ya mimba zote. Kichefuchefu na kutapika zinaweza kuwa moja kati ya ishara za kwanza za mimba na kwa kawaida huanza wiki ya 6 ya mimba (wiki ya 1 kuanzia siku ambayo kipindi cha mwisho kilianza). Inaweza kutokea wakati wowote wa siku, na kwa wanawake wengi huonekana kuisha wiki ya 12 ya mimba.
Sababu
[hariri | hariri chanzo]Sababu za ugonjwa wa asubuhi ni pamoja na:
- Ongezeko la mzunguko wa homoni ya estrogen. Viwango vya Estrogen vinaweza kuongezeka hadi mia wakati wa ujauzito. Hata hivyo, hakuna ushahidi thabiti ya tofauti katika viwango vya estrogen kati ya wanawake ambao huugua kutokana na ugonjwa huu na wale ambao hawaugui.
- Kuwa na sukari kidogo kwa damu (hypoglycemia) kutokana na nishati inayovutwa na plasenta kutoka kwa mama mja mzito, ingawa bado masomo haijathibitisha hii.
- Ongezeko la "progesterone" hupumzisha misuli katika uterasi, ambayo huzuia kujifungua mapema, lakini inaweza pia kupumzisha tumbo na matumbo, na kupelekea kuzidi kwa asidi za tumbo na ugonjwa wa astroesophageal reflux.
- Ongezeko katika human "chorionic gonadotropin".
- Ongezeko katika kuhisi harufu, ambayo huanzisha uchochezi zaidi wa kichefuchefu ya kawaida.
Ugonjwa wa asubuhi kama njia ya kinga
[hariri | hariri chanzo]Ugonjwa wa asubuhi kwa sasa unaeleweka kama tabia ambayo inalinda mtoto tumboni dhidi ya sumu au toksi zinazomezwa na mama mjamzito. Mimea mingi ina kemikali zenye sumu ambazo haziwezi kuliwa. Binadamu wazima, kama wanyama wengine, wana ulinzi dhidi ya sumu za mimea, pamoja na "enzyme" zilizotengenezwa kwa ini ambazo hutumiwa kutoa makali ya sumu na tishu za viungo vingine mbalimbali ndani ya mwili. Katika mimba, walinzi bado hawajakomaa kikamilifu, na hata dozi ndogo za sumu kutoka kwa mimea ambazo athari yake si hatari sana kwa watu wazima zinaweza kudhuru mtoto. Ugonjwa wa mimba husababisha wanawake kuhisi kichefuchefu wakati wamenusa au kuonja vyakula ambavyo vina uwezekano wa kuwa na sumu ambazo zaweza kudhuru fetus, ingawa zinaweza kutowadhuru.
Kuna ushahidi wa kutosha kuiunga mkono nadharia hii, kama:
- Ugonjwa wa asubuhi kwa kawaida huwa miongoni mwa wanawake wajawazito. Nadharia hii ina neema kuwa ugonjwa wa asubuhi ni hali ya kawaida dhidi ya wazo kwamba ni ugonjwa.
- Kutoweza kujikinga kwa mtoto hufikia kilele chake baada ya miezi 3, ambayo pia ni wakati wa kilele cha kuhisi ugonjwa wa asubuhi.
- Kuna uwiano mzuri kati ya ukolezi wa sumu katika vyakula, na ladha na harufu ambazo husababisha damu au chakula kutoka sehemu moja ya mwili hadi nyingine
- Wanawake ambao hawana ugonjwa wa asubuhi wana uwezekano mkubwa wa kupoteza mimba au kuwazaa watoto wenye shida za kuzaliwa.
Ugonjwa wa asubuhi haumlindi tu mtoto ambaye angali katika tumbo la mama yake bali pia mjamzito mwenyewe. Mfumo wa kingamaradhi (immune system) wa wanawake wajawazito huzuiwa au husimamishwa wakati wa ujauzito, labda kupunguza uwezekano wa kuzikataa tishu za dhuriya zao wenyewe. Kwa sababu hii, bidhaa za wanyama ambazo zina vimelea na bakteria ambazo zina madhara zinaweza kuwa hatari hasa kwa wanawake wajawazito. Kuna ushahidi kuwa ugonjwa wa asubuhi husababishwa mara nyingi na bidhaa za wanyama kama vile nyama na samaki.
Kama ugonjwa wa asubuhi ni mfumo wa ulinzi dhidi ya usindikaji wa sumu tumboni, kupatiana kwa dawa za kupambana na kichefuchefu kwa wanawake wajawazito kunaweza kuwa na athari za kando kama kusababisha kasoro wakati wa kuzaa au kupoteza mimba kwa kuhimiza maamuzi ya chakula yanayodhuru. Kwa upande mwingine, mboga nyingi za kienyeji zimepandwa makusudi kuwa na kiwango kidogo cha toksini kuliko katika kipindi cha kitambo, na hivyo kiwango cha tishio kwa mtoto si cha juu kama ilivyokuwa wakati mfumo wa ulinzi ulivyonaza.
Maelezo mengine
[hariri | hariri chanzo]Nadharia zingine zisizo za kisayansi za ugonjwa wa asubuhi zimependekezwa hapo awali. Kulingana na msaikolojia Sigmund Freud, imeonekana kuwa ugonjwa wa asubuhi ni matokeo ya mama kutokuwa na hisia au hamu kwa mumewe. Udhihirisho huu ni hamu ya kuavya mimba kwa kutapika. Kwa ujumla, nadharia hizi zimekanushwa au zimekataliwa na wanasayansi wa kisasa; Steven Pinker, katika kitabu chake "How the Mind Works " huenda zaidi, hufanyia mzaha wazo hili kama nadharia ya " barf-up-your-baby ".
Matibabu
[hariri | hariri chanzo]Matibabu ya ugonjwa wa asubuhi hulenga kupunguza dalili za kichefuchefu, badala ya kushambulia mizizi ambazo husababisha kichefuchefu. Matibabu hujumuisha:
- Ndimu, hasa kunusa ndimu iliyokatwa.
- Kuepuka tumbo tupu (kuepuka njaa).
- Kuwa na uwezo wa kukubali au kukataa aina tofauti ya vyakula.
- Kula milo ndogo mara tatu au sita kwa siku, badala ya tatu kubwa.
- Kula kabeji. [1]
- Kujaribu mlo wa BRAT (Bananas, Rice, AppleSauce na Tea): ndizi, mchele, mchuzi wa tofuti, tosti na chai.
- Tangawizi, katika vidonge, chai, au tangawizi hani.
- Kula kavu "crackers" asubuhi.
- Unywaji wa vioevu dakika 30-45 baada ya kula chakula ngumu.
- Kama vioevu vitatapikwa, inapendekezwa kunyonya barafu zilizotengenzwa kutoka kwa juisi ya matunda au maji.
- Vitamini B6 (aidha pyridoxine au pyridoxamine), mara nyingi huliwa pamoja na antihistamine doxylamine (Diclectin).
Daktari anaweza kuagiza dawa za kupambana na kichefuchefu kama mama mtarajia hutaabika kutokana na upungufu wa maji mwilini au utapiamlo kama matokeo ya ugonjwa wake wa asubuhi, hali inayojulikana kama hyperemesis gravidarum . Nchini Marekani, Zofran (ondansetron) kwa kawaida ndiyo dawa ya uchaguzi, ingawa gharama yake ya juu ni kizuizi kwa baadhi ya wanawake; nchini Uingereza, madawa ya zamani ambayo yana uzoefu mkubwa katika mimba hupendelewa promethazine likiwa chaguo la kwanza na vinginevyo kama metoclopramid, au prochlorperazine vikiwa chaguo ya pili.
Thalidomide
[hariri | hariri chanzo]Thalidomide ilitengenezwa na kuagizwa kama tiba ya ugonjwa wa asubuhi nchini Ujerumani ya Magharibi, lakini matumizi yake ilikomeshwa wakati athari za dawa hiyo zilipojulikana. "United States Food and Drug Administration" kamwe halikukubali thalidomide kwa matumizi ya kutibu ugonjwa wa asubuhi.
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]- ↑ Akhtar MS, Munir M (1989). "Evaluation of the gastric anti-ulcerogenic effects of Solanum nigrum, Brassica oleracea and Ocimum basilicum in rats". 27: 163–176. PMID 2515396.
Brassica oleracea (leaf) powder did not affect the ulcer index significantly but its aqueous extract lowered the index and increased hexosamine levels, suggesting gastric mucosal protection.
{{cite journal}}
: Cite journal requires|journal=
(help)
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Morning Sickness: A Comprehensive Guide to the Causes and Treatments, Nicky Wesson, Vermilion (1997), ISBN 0-09-181538-X
- Morning Sickness - A Medical Dictionary, Bibliography, and Annotated Research Guide to Internet References, ICON Health Publications (2004), ISBN 0-597-84043-1