Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1960
Mandhari
Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1960 ulikuwa wa 44 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 8 Novemba. Upande wa "Democratic Party", mgombea John F. Kenndy (pamoja na kaimu wake Lyndon B. Johnson) alimshinda mgombea wa "Republican Party" Richard Nixon (pamoja na kaimu wake Henry Cabot Lodge).
Uchaguzi huo ulikuwa wa kwanza wa majimbo hamsini, yaani wachaguzi kutoka Alaska na Hawaii waliruhusiwa mara ya kwanza.
Matokeo
[hariri | hariri chanzo]Kennedy akapata kura 303, na Nixon 219 wakati kura 15 zilipigiwa kwa Harry F. Byrd asiyegombea. Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |