Nenda kwa yaliyomo

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, 1948

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Uchaguzi wa Rais wa Marekani, mwaka wa 1948 ulikuwa wa 41 katika historia ya Marekani. Ukafanywa Jumanne tarehe 2 Novemba. Upande wa "Democratic Party", Rais Harry S. Truman (pamoja na kaimu wake Alben Barkley) aliwashinda mgombea wa "Republican Party" Thomas E. Dewey (pamoja na kaimu wake Earl Warren) na mgombea Strom Thurmond (pamoja na kaimu wake Fielding L. Wright).

Truman akapata kura 303, Dewey 189 na Thurmond 39 (pamoja na kura moja kutoka Tennessee iliyopigiwa kwake badala ya kwa Truman). Ramani yaonyesha kura kwa kila jimbo.