Uambukizo wa chawa kichwani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Head lice infestation (pediculosis capitis)
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyInfectious diseases Edit this on Wikidata
ICD-10B85.0
DiseasesDB9725
MedlinePlus000840
eMedicinemed/1769
MeSHD010373

Uambukizo wa chawa kichwani (pia inajulikana kama pediculosiscapitis,[1] mayai ya chawa,[2] au chawa[3]) ni maambukizi ya nywele ya kichwa na skalpu na chawa wa kichwa (Pediculus humanus capitis).[4] mwasho kutokana na kuumwa na chawa ni ya kawaida.[5] Wakati wa maambukizi ya kwanza ya mtu, mwasho inaweza kukosa kutokea hadi wiki sita.[5] Ikiwa mtu ataambukizwa tena, dalili zinaweza kuanza tena haraka.[5] Mwasho unaweza kusababisha matatizo ya kulala.[6] Kwa kawaida, hata hivyo, sio hali iliyo hatari sana.[7] Ilhali chawa inaonekana kusambaza magonjwa mengine nchini Afrika, hawaonekani kufanya hivyo barani Ulaya au Amerika Kaskazini.[4][6]

Kisababishi na utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Chawa husamabazwa kwa kugusana moja kwa moja na nywele ya mtu aliyeambukizwa.[6] Kisababishi cha uambukizo wa chawa kichwani haihusiani na hali ya usafi.[5] Wanyama wengine, kama vile paka na mbwa, hawachangi usambazaji.[6] Chawa hula tu damu ya binadamu na wanaweza kuhisi tu kwa nywele ya binadamu.[4][5] Wakiwa wakubwa, wako na urefu wa karibu milimita 2 hadi 3.[8] Wakati hawako kwa binadamu hawawezi kuhisi zaidi ya siku tatu.[5] Binadamu anaweza pia kuambukizwa aina mbili za chawa – chawa wa mwili na chawa wa sehemu za jenitalia. Ili kufanya utambuzi, ni lazima chawa aliyehai apatikane.[5] Ukitumia kichana inaweza kusaidia kupata.[5] Makaka ya mayai yaliyowazi (inajulikana kama mayai ya chawa) hayatoshi kwa utambuzi.[5]

Matibabu[hariri | hariri chanzo]

Uwezekano wa matibabu inajumuisha: kuchana nywele kila wakati na kichana kizuri au kunyoa kichwa kabisa. Baadhi ya matibabu yajuu ya mwili ni salama pia, ikiwemo malathion, invermectin, na dimeticone.[7] Dimeticone, ambayo ni mafuta ya silicone, hupendelewa sana kwa sababu ya athari ya chini.[7] Pyrethroidkama vile permethrin yametumiwa sana; hata hivyo, yamekuwa na faida ya chini kwa sababu ya ongezeko la pingamizi.[7] Hii ni ushahidi kidogo wa dawa mbadala.[9]

Epidemiolojia, historia, jamii na utamaduni[hariri | hariri chanzo]

-Maambukizi ya kichwa ya chawa ni kawaida, haswa kwa watoto.[5] Barani Ulaya, wanaambukiza kati ya asilimia 1 na 20 ya vikundi tofauti ya watu.[4] Nchini Marekani, kati ya watoto milioni 6 hadi 12 wanaambukizwa kwa mwaka.[6] Hutokea mara nyingi kwa wasichana kuliko wavulana.[5] Imependekezwa kihistoria, kuwa maambukizi ya kichwa na chawa ilikuwa na manufaa, walipokuwa wanazuia dhidi ya chawa wa mwili walio hatari zaidi.[10] Maambukizi inaweza kusababisha unyanyapaa kwa watu walioambukizwa.[5]

Marejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. Rapini, Ronald P.; Bolognia, Jean L.; Jorizzo, Joseph L. (2007). Dermatology: 2-Volume Set. St. Louis: Mosby. ISBN 1-4160-2999-0. 
  2. "How to treat nits". nhs.uk. 2012-09-14. Iliwekwa mnamo 23 October 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  3. "cootie". http://dictionary.reference.com/. Iliwekwa mnamo 23 October 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 Feldmeier, H (Sep 2012). "Pediculosis capitis: new insights into epidemiology, diagnosis and treatment.". European Journal of Clinical Microbiology & Infectious Diseases 31 (9): 2105–10. PMID 22382818. doi:10.1007/s10096-012-1575-0. 
  5. 5.00 5.01 5.02 5.03 5.04 5.05 5.06 5.07 5.08 5.09 5.10 5.11 Smith, CH; Goldman, RD (Aug 2012). "An incurable itch: head lice.". Canadian family physician Medecin de famille canadien 58 (8): 839–41. PMID 22893334.  Check date values in: |date= (help)
  6. 6.0 6.1 6.2 6.3 6.4 "Parasites - Lice - Head Lice Frequently Asked Questions (FAQs)". cdc.gov. September 24, 2013. Iliwekwa mnamo 23 October 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  7. 7.0 7.1 7.2 7.3 "Head lice. Dimeticone ni chaguo la pediculicide.". Prescrire Int. 151 (23): 187–90. Jul 2014. PMID 25162097. 
  8. "Parasites - Lice - Head Lice". cdc.gov. September 24, 2013. Iliwekwa mnamo 23 October 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  9. Takano-Lee M, Edman JD, Mullens BA, Clark JM (December 2004). "Home remedies to control head lice: assessment of home remedies to control the human head louse, Pediculus humanus capitis (Anoplura: Pediculidae)". Journal of Pediatric Nursing 19 (6): 393–8. PMID 15637580. doi:10.1016/j.pedn.2004.11.002.  Check date values in: |date= (help)
  10. Rózsa, L; Apari, P (May 2012). "Why infest the loved ones--inherent human behaviour indicates former mutualism with head lice.". Parasitology 139 (6): 696–700. PMID 22309598. doi:10.1017/S0031182012000017.  Check date values in: |date= (help)