Tuta la mchanga 45

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Tuta 45

Tuta la Mchanga 45 (ing. dune 45) ni kilima cha mchanga huko Sossusvlei nchini Namibia kilichojengwa na upepo kwa kupuliza na kusukuma punje za mchanga. Asili ya mchanga huu ni mwendo wa mto Oranje uliosagasaga mwamba njiani mwake kwenye mwendo wa miaka mamilioni, kuupeleka mchanga hadi bahari Atlantiki ambako mawimbi yameurudisha kwenye pwani upande wa kaskazini. Kutoka mwambao wa bahari upepo unasukuma punje za mchanga kuelekea barani zinapojenga matuta ya mchanga. Hili tuta la mchanga 45 limepokea jina kutokana na mahali pake kwenye kilomita namba 45 ya barabara inayopita karibu. Kwa sababu ya umbo wake wa ajabu Tuta la Mchanga 45 unapokea maelfu za watalii kila mwaka.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Anwani ya kijiografia: 24°43′S 15°28′E / 24.717°S 15.467°E / -24.717; 15.467