Nenda kwa yaliyomo

Turubali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kijana akifurahia mchezo huu.

Turubali ni kifaa kinachotumika kwa mchezo ujulikanao kwa lugha ya Kiingereza kama Trampoline.

Turubali huwa na kipande cha nguo nzito iliyotandazwa juu ya chuma na chini yake kukawekwa springi. Kirukio hutumika kwa kujifurahisha wakati unaporuka. Huenda pia turubali ikatumika kwa mashindano ya kubaini atakayeruka juu zaidi kuliko mwenzake.

Nguo ambayo mtu hurukia kwa turubali haina uwezo wa kumfanya aweze kurukaruka. Springi zilizo chini ya hio nguo ndizo zilizo na uwezo ule wa kumfanya mtu arukeruke.

Historia ya turubali

[hariri | hariri chanzo]

Mchezo unaofanana na ule wa turubali ulianzishwa na watu wa Inuit. Walikuwa wakiwarusha wanadensi kwa hewa mtu mmoja baada ya mwingine. Kuna ushahidi pia kuwa watu wa Uropa walikuwa wakirushwa juu na wenzao kwa kutumia blanketi kama adhabu.

Kuna ushahidi pia ya wazima moto kutumia aina ya virukio kuwashika waliokuwa wakipotea moto kwa ghorofa za juu mwaka wa 1887.

Uvumbuzi wa turubali ya kisasa

[hariri | hariri chanzo]

Turubali ya kwanza ya kisasa kama tunavyoijua leo ilivumbuliwa na George Nissen na Larry Griswold mwakani 1936.

Usalama wa turubali

[hariri | hariri chanzo]

Utumizi wa turubali waweza kuwa na ajali zake. Yafaa kirukio kiwe na povu ili unaporukaruka usije ukaanguka kwa chuma na kuumia vibaya.

Kulingana na kikundi cha madakatri wa watoto nchini Amerika, kirukio chafaa kutumiwa kwa uangalifu mwingi. Wanakanya kuwa watoto walio chini ya umri wa miaka sita wasitumie kirukio.

Mengine ya kuzingatia kuhakikisha kuwa kirukio chatumika kwa usalama ni kama:

1.      Kuwa watoto wasifanye mitindo inayoweza wahatarisha

2.      Kuwepo na mtu mzima wa kusimamia watoto wanaporukaruka kwa turubali

3.      Kwa kila wakati iwe ni mtoto mmoja tu anayerukaruka kwa turubali

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
  1. History of trampolines
  2. Trampolines can cause serious injuries
  3. .Are trampolines safe for toddlers
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu zaidi kuhusu Turubali kama historia yake, uenezi au kanuni zake?
Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.