Nenda kwa yaliyomo

Chuo Kikuu cha Tumaini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Tumaini University)

Chuo Kikuu cha Tumaini ni taasisi ya mafunzo ya juu nchini Tanzania iliyopo chini ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Matawi ya Chuo Kikuu Tumaini

[hariri | hariri chanzo]

Chuo kikuu Tumaini kina matawi manne:

Tawi la kwanza lilikuwa Chuo cha Theolojia Makumira huko Usa River, (Arusha) kilichoanzishwa mwaka 1947 kama mahali pa mafunzo kwa ajili ya wachungaji wa kanisa.

Tawi la pili liko Moshi mjini lajulikana hasa kama Kilimanjaro Christian Medical College (KCMC). Kilianzishwa mwaka 1971 kama hospitali ya Kikristo ya rufaa na ya kufundisha waganga.

Tawi la tatu lipo Iringa. Chuo kilianzishwa 1993 kwa jina la Chuo cha Kilutheri cha Iringa. Tangu 1995 masomo mbalimbali yaliongezwa: tangu 1995 biashara, tangu 1997 uandishi habari, tangu 1998 sheria, tangu 2001 ualimu. Vyeti vya kwanza vya bachelor vikatolewa 1998.

Tawi la nne lipo Dar es Salaam ambalo lilifunguliwa hivi karibuni.

Kuanzishwa kwa Chuo Kikuu 1996

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 1996 vyuo vitatu vilivyokuwepo viliunganisha kuwa chuo kikuu cha kitaifa cha kilutheri. Azimio hili lilifuata sheria ya Tanzania na. 10 ya 1995 iliyoruhusu taasisi zisizo za kiserikali.

Makao makuu yapo KCMC Moshi.

Askofu Mkuu wa KKKT huwa ni Chansella wa Chuo Kikuu. Chansella wa chuo hiki hivi sasa ni Dr. Samson Mushemba. Makamu wa chansella ni pofesa John F. Shao.


Viungo vya Nje

[hariri | hariri chanzo]