Nenda kwa yaliyomo

Trevor Graham

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Trevor Graham ni mzaliwa wa Jamaika na ni kocha wa zamani wa riadha ana makao yake Marekani. Kufuatia kashfa ya BALCO, Kamati ya Olimpiki ya Marekani ilimfukuza kutoka viwanja vyao vyote vya mazoezi kwa sababu wanariadha wake kadhaa walikuwa wamepimwa na kupatikana kuwa wanatumia dawa haramu.

Wasifu kama mwanariadha

[hariri | hariri chanzo]

Graham alikuwa katika timu ya Jamaika ya mbio ya 4 x 400m iliyoshinda medali ya fedha katika Olimpiki ya 1988,alipokimbia katika awamu ya kwanza ya kuhitimu na nusu fainali lakini hakushiriki katika fainali. Yeye alihitimu digrii katika Umeneja wa Biashara kutoka Chuo cha Saint Augustine.

Wasifu wa Kocha

[hariri | hariri chanzo]

Sprint Capitol USA

[hariri | hariri chanzo]

Ikiwa imeanzishwa mwaka wa 1993 na Graham na ikakubaliwa katika mwaka wa 1997, Sprint Capitol USA ilikuwa na makao yake katika Treki ya Paul Derr katika Chuo Kikuu cha Carolina Kaskazini huko Raleigh,Carolina Kaskazini.

Miongoni mwa wanariadha ambao walijiunga na mafunzo ya kikundi hiki walikuwa:

  • Shawn Crawford
  • Justin Gatlin - aliyekatazwa ushiriki kwa miaka minane na USADA katika mwaka wa 20006.
  • Alvin Harrison - aliyekatazwa ushiriki kwa miaka minne na USADA tangu 2004.
  • CJ Hunter - alipatikana na Nandrolone baada ya kujitoa kutoka Olimpiki ya 2000.
  • Marion Jones - medali zote na rekodi zote zilitupiliwa mbali baada ya kukubali utumiaji wa dawa za kuboresha utendaji katika kasfa ya BALCO.
  • Tim Montgomery - Rekodi ya 100m ilitupiliwa mbali baada ya kukubali kuwa alitumia dawa za kuboresha utendaji kutoka BALCO.
  • Antonio Pettigrew - medali zote za timu ya 4 x 400m ya Marekani ya Olimpiki ya 2000 zilichukuliwa baada ya Antonio kukubali kuwa alitumia dawa za HGH na EPO.
  • Jerome Young - alikatazwa ushiriki lakini hukumu hii ilipinduliwa.
  • Marcus Brunson
  • Duane Ross
  • Randall Evans
  • Chandra Sturrup
  • Me'Lisa Barber
  • LaTasha Jenkins

Kashfa ya BALCO

[hariri | hariri chanzo]

Graham alikuwa na jukumu muhimu katika kashfa ya BALCO(Bay Area Laboratory Co-operative) wa mwezi wa Juni 2003, alipotuma(bila kufichua yeye ndiye aliyetuma) sindano yenye Tetrahaidrogenistrinone(kwa ufupi THG) kwa anwani ya Kituo cha Marekani ya kupigana dhidi ya dawa haramu(United States Anti-Doping Agency). Mnamo Julai 2006, Angel Guillermo Heredia alitoa ushahidi mbele ya US Federal Grand Jury akisema kuwa alifanya kazi chini ya Graham kwa miaka ya 1996 - 2000 akimsambazia dawa haramu. Ingawa baadhi ya wanariadha aliyekuwa kocha wao wameshutumiwa kwa utumiaji wa dawa hizo haramu ,yeye hukana kuhusika ama kujua lolote na pia husema hamjui Heredia. Baada ya Gatlin kufeli majaribio ya kisayansi ya testosteroni.hii ilitangazwa mnamo mwezi Julai 2006,Graham alisema katika mahojiano kuwa Gatlin alikuwa amewekewa kosa la uongo.

Barua ,ambayo haikutumwa, iliyoandikwa na Victor Conte wa BALCO kwa U.S. Anti-Doping Agency ilieleza utumiaji wa testosteroni ya kumezwa na Graham ambayo "ingetoka mwilini na haipatikani katika mkojo katika majaribio ya kisayansi baada ya siku chache" Katika mwisho wa barua hiyo,Gatlin alikuwa mmojawapo wa wanariadha wanne waliotambuliwa kuwa walitumia dawa hiyo.

IAAF ilisema mnamo 31 Julai,2006 kuwa Graham angekatazwa kushiriki katika riadha iwapo ushahidi wowote ungemhusisha na kuvunjwa kwa sheria za utumiaji dawa haramu na United States Anti-Doping Agency ishindwe kufanya lolote.

Tarehe 3 Agosti 2006 na Kamati ya Olimpiki ya Marekani ilipiga marufuku Trevor Graham kutoka kutumia vituo vyake vya mafunzo. [18] Hii ilikuwa mara ya kwanza kwa kocha kupata hukumu kama hiyo kwa sababu ya idadi kubwa ya wanariadha waliokuwa wakifunzwa na yeye kupatikana na dawa haramu. Kama matokeo ya hayo, Nike ilimaliza mkataba wake na Graham katika mwezi wa Agosti 2006. [20]

Tarehe 29 Mei 2008, Graham mara moja alipatikana na hatia ya kuwadanganya wapelelezi wa kesi hiyo. Kesi ilishindwa kufungwa mara mbili baada ya kamati ya kuhukumu iliposhindwa na kutoa uamuzi mmoja.

Mkuu wa United States Anti-Doping Agency,Travis Tygar, mnamo 15 Julai 2008, alithibitisha kupigwa marufuku kutoka riadha kwa maisha yake yote , Trevor Graham baada ya kuvunja sheria:"Hii inawasilisha ujumbe kuwa makocha pia wako chini ya sheria. Kuna wazo kuwa wako juu ya sheria kwa sababu hatuwapimi lakini hii sasa inaonyesha tutatumia mamlaka zetu zote. Hakuna nafasi ya kutafuta kurudishwa kazi. Nafasi yoyote yake ya kufanya hivyo ilipita. Kupigwa marufuku kwake kulihusu pia matukio yoyote yaliyoandaliwa na Kamati ya Olimpiki ya Marekani,IAAF na USA Track & Field na vikundi vingine vyote vilivyohusika katika mpango wa World Anti-Doping Agency.

Wanariadha waliojiunga na Sprint Capitol USA

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Results of 1988 Seoul Summer Olympic Game: Athletics – 4x400m relay Men: Round 1". Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. Japan Institute of Sports Sciences.
  2. "Results of 1988 Seoul Summer Olympic Game: Athletics – 4x400m relay Men: Semi-final". Ilihifadhiwa 28 Septemba 2007 kwenye Wayback Machine. Japan Institute of Sports Sciences.
  3. "Sprint Capitol, USA - Coaches & Staff" Ilihifadhiwa 29 Mei 2014 kwenye Wayback Machine.. Sprint Capitol USA. 2005.
  4. Mackay, Duncan (2006-07-31). "Gatlin turns into the fastest falling hero in the world". The Guardian. .
  5. Wilson, Duff (2006-07-20). "Instigator of Steroids Inquiry May Be a Target". New York Times.
  6. Pells, Eddie (2006-07-31). "Gatlin set up: coach". Associated Press (Globe and Mail).
  7. "IAAF: Gatlin's coach might face two-year ban". Associated Press. 2006-08-07.
  8. "USOC bans track coach Graham from training sites". Associated Press. 2006-08-07.
  9. "Nike ends contract with track coach Graham". Associated Press. 2006-08-25.
  10. [https://web.archive.org/web/20090215015004/http://hosted.ap.org/dynamic/stories/A/ATHLETES_STEROIDS?SITE=FLTAM&SECTION=SPORTS&TEMPLATE=DEFAULT Dubow, Josh; Paul Elias and Raf Casert (2008-05-30). "Track coach Graham convicted in BALCO probe". Tampa Bay Online.
  11. bbc.co.uk, Coach Graham is handed life ban
  12. Track coach Trevor Graham gets banned for life