Tommy Olivencia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tommy Olivencia (jina la kuzaliwa: Ángel Tomás Olivencia Pagán; 15 Mei 1938 - 22 Septemba 2006) alikuwa kiongozi maarufu wa bendi ya muziki ya salsa nchini Puerto Rico.[1]

Maisha ya awali[hariri | hariri chanzo]

Olivencia alizaliwa huko Villa Palmeras ya Santurce, San Juan, Puerto Rico. Familia yake ilihamia jiji la Arecibo pindi alipokuwa mtoto. Alipata elimu yake ya msingi na ya sekondari huko. Akiwa kijana, alivutiwa sana na tarumbeta na akajifunza kupiga ala hiyo ya muziki. Mwaka wa 1954, Olivencia aliimba na kupiga tarumbeta kwenye bendi mbalimbali . Alihitimu shule ya sekondari mwaka 1957 na familia yake ilihamia tena Santurce.[2]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tommy Olivencia kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.