Timu ya taifa ya Kenya ya raga ya wachezaji saba
Timu ya taifa ya Kenya ya raga ya wachezaji saba hushiriki katika mashindano ya IRB Sevens World Series na shindano la kombe la dunia ya raga ya wachezaji saba. Kwa sasa ni moja kati ya timu 12 muhimu ya IRB Sevens walio na uhakika wa kushiriki mahali matukio yote nane yanafanyika kila msimu.
Historia
[hariri | hariri chanzo]Timu ya Kenya ya raga ya wachezaji saba inashiriki katika mashindano ya kimataifa ya raga ya wachezaji saba na imekuwa na mafanikio zaidi kuliko wenzao wanaocheza raga ya wachezaji kumina tano. Umaarufu wao kuu ya kwanza katika mashindano ya raga ya wachezaji saba ilikuwa kuishinda timu ya Australia katika London Sevens 2006, walipoendelea kufika finali ya ushindani wa Bamba. Katika mashindano ya Wellington Sevens mwaka 2007 nchini New Zealand, Kenya ilikuwa nambari ya pili katika kundi lao, ikishinda timu kubwa kama Ajentina na Tonga, kabla ya kushindwa katika robo-fainali na timu ambaye hatimaye ilikuwa ya pili, Fiji.
Kenya imeimarika haswa katika msimu wa raga wa wachezaji saba katika mwaka wa 2008-09. Wao walifika nusu fainali katika Kombe la Dunia mwaka wa 2009 , hatimaye wakishindwa na Ajentina. Katika mashindano ya IRB mwaka ya mwaka huo, Kenya ilifikia fainali za Kombe kuu kwa mara ya kwanza katika shindano lililokuwa Adelaide , lakini walishindwa na Afrika ya Kusini katika Finali; |Katika mashindano ya IRB mwaka ya mwaka huo, Kenya ilifikia fainali za Kombe kuu kwa mara ya kwanza katika shindano lililokuwa Adelaide , lakini walishindwa na Afrika ya Kusini katika Finali; [1] wao walishiriki katika nusu finali mara mbili katika matukio mengine.
Tuzo
[hariri | hariri chanzo]- Nambari mbili katika shindano la Bamba katika mashindano yalikuwa jijini London mwaka wa 2006. Wao walishindwa 42-7 katika fainali Afrika Kusini lakini waliwashinda Australia 26-7 katika njia yao ya kuelekea finali.
- Washindi wa shindano la Bamba mwaka wa2007 katika mashindano nchini Afrika ya Kusini, waliwashinda wahiriki wa mshangao Marekani 15-14 katika fainali.
- Ilishinda Timu ya Mwaka katika jamii ya wanaume katika tuzo la Kenya Sports Personality of the year mara nne: katika mwaka wa 2004, 2007, 2008 na 2009 [2]
Wachezaji maarufu
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ IRB, 5 Aprili 2009: Afrika ya Kusini kurejesha Adelaide Sevens Archived 8 Aprili 2009 at the Wayback Machine.
- ↑ "Soya Awards - 2007 winners". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-09-13. Iliwekwa mnamo 2009-12-16.
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Timu ya taifa ya Kenya ya raga ya wachezaji saba kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |