Nenda kwa yaliyomo

Timi Dakolo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha ya Timi Dakolo

Timi Dakolo (amezaliwa 20 Januari 1981) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, na mtayarishaji wa muziki wa Nigeria.[1]

Maisha ya Awali

[hariri | hariri chanzo]

Timi Dakolo alizaliwa mjini Accra, Ghana kwa baba yake Mnaijeria aitwaye David kutoka jimbo la Bayelsa na mama yake Mgana, Norah Kimmy Head, ambaye alifariki wakati Dakolo akiwa na umri wa miaka kumi na tatu.[2] Licha ya kuzaliwa Ghana, Timi ana pasipoti ya Nigeria na hakudai uraia wa nchi mbili. Alilelewa mjini Port Harcourt na bibi yake Ateni Dakolo pamoja na shangazi yake Susan Larry, ambaye pia alimfundisha kuimba. Uhusiano wao ulikuwa wa karibu kiasi kwamba Timi alikataa ofa ya kuhamia Lagos na wazazi wake, akiamua kubaki Port Harcourt pamoja nao.

Timi alianza kuimba kanisani akiwa na umri wa miaka kumi na mbili. Mnamo mwaka 2003, alijiunga na kundi la muziki Purple Love akiwa miongoni mwa waanzilishi. Kundi hili lilitamba katika kumbi za burudani za Port Harcourt, lakini lilivunjika mwaka 2005 baada ya wanakikundi wote kupata nafasi ya kujiunga na Chuo Kikuu cha Port Harcourt. Katika kipindi hicho pia, Timi alishinda shindano la utafutaji vipaji la kienyeji lililojulikana kama G.E FACTO lililofanyika Port Harcourt.


  1. "Why I fear for the future of my children —Timi Dakolo". Tribune Online (kwa Kiingereza (Uingereza)). Mei 9, 2021. Iliwekwa mnamo 2022-03-19.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Waves of Timi Dakolo at 40". THISDAYLIVE (kwa American English). 23 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 19 Machi 2022.
Makala hii kuhusu mwanamuziki fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Timi Dakolo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.