Thishiwe Ziqubu
Thishiwe Ziqubu (amezaliwa 5 Agosti 1985) ni mkurugenzi, mwandishi na mwigizaji wa filamu wa Afrika Kusini.[1] Alishinda Tuzo ya Africa Movie Academy ya Mwigizaji msaidizi bora mnamo mwaka 2016, kupitia filamu aliyoshiriki kama Tashaka, filamu hii ya vichekesho vya mapenzi inajulikana kwa jina la Tell Me Sweet Something.[2] Mnamo mwaka 2019, aliongoza vipindi vya maigizo vya MTV Shuga.
Elimu
[hariri | hariri chanzo]Ziqubu alisomea Uandishi na Uelekezaji baada ya shule ya upili. Baadaye alihudhuria Chuo cha Filamu na Maigizo cha Afrika (AFDA).Alikamilisha pia Elimu yake ya Uigizaji katika chuo cha Los Angeles cha New York Film Academy.[1]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Ziqubu alijitokeza kwa mara ya kwanza mwaka 2011 katika filamu ya Man on Ground,ambayo ilimsaidia kusonga mbele katika kazi yake.Kama mwandishi na mkurugenzi, aliandika na kuelekeza filamu fupi tatu huru ambazo ni Out Of Luck, Subdued na Between the Lines.[1].Pia ameshiriki kuandika tamthiliya za televisheni za Afrika Kusini ikiwemo Isidingo,Rhythm City na Is'Thunzi ni mfululizo wa maigizo.Pia alishiriki kama mwandishi mkuu na kuelekeza katika safu ya maigizo yenye sehemu nne inayoitwa Emoyeni.
Mnamo mwaka 2019, aliongoza vipindi vya msimu wa pili wa safu ya Runinga MTV Shuga.[3]
Baadhi ya Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina | Uhusika |
---|---|---|
2011 | Man on Ground | Zodwa |
2014 | Hard to get | Skiets[4] |
2015 | While You Weren't Looking | Shado |
2015 | Tell Me Sweet Something | Tashaka |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ 1.0 1.1 1.2 Bongiwe Sithole. "The Rise and rise of Thishiwe Ziqubu", The Sowetan, 6 February 2016. Retrieved on 13 June 2016.
- ↑ Albert Benefo Buabeng. "Full list of winners at 2016 Africa Movie Academy Awards", Pulse Ghana, 12 June 2016. Retrieved on 13 June 2016. Archived from the original on 2017-04-30.
- ↑ MTV Shuga (14 Februari 2019), MTV Shuga: Down South (S2) - The Preview Show, iliwekwa mnamo 19 Februari 2019
{{citation}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Helen Herimbi. "A new girl Nox on Kilowatt’s door", e.tv, 10 March 2015. Retrieved on 13 June 2016.
Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Thishiwe Ziqubu kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |