The Era (gazeti)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
The Era
Bango la Toleo la Kwanza katika mwaka wa 1838
Jina la gazeti The Era
Aina ya gazeti Gazeti la kuchapishwa kila siku
Lilianzishwa 1838
Eneo la kuchapishwa Uingereza
Nchi Uingereza
Mhariri *. Leitch Ritchie (Mhariri wa kwanza)
*. Frederick Ledger (Mhariri wa pili)
Lilikwisha 1939

The Era lilikuwa gazeti la Uingereza la kuchapishwa kila wiki, lilichapishwa kutoka mwaka wa 1838 hadi 1939. Hapo awali, lilikuwa gazeti la habari ya jumla lakini likajulikana kwa habari yake ya michezo na ,hapo baadaye, habari zake za maigizo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

The Era ilianzishwa katika mwaka wa 1838 na muungano wa wanahisa ,baadhi yao waliokuwa wasambazaji wa bidhaa na watu wengine waliohusika na biashara yao. Jarida hili lilikuwa likilengwa kuwa chombo cha kuwasilisha habari ya kila wiki kama vile gazeti la Morning Advertiser lilivyokuwa chombo cha kutumika kila siku. Katika miaka miwili mitatu hivi ya kuwepo kwa gazeti hili, msimamo wake wa kisiasa ulikuwa wa kukubali siasa yoyote. Mhariri wake wa kwanza, Leitch Ritchie, alionekana kuwa huru sana na bodi ya wakurugenzi na kuongezea migogoro ya wahariri, gazeti hilo lilifeli. Frederick Ledger alichukua nafasi ya Ritchie na akawa mwendeshaji pekee na, vilevile, mhariri wa gazeti hilo. Alihariri jarida hili kwa zaidi ya miaka thelathini, likibadilisha siasa yake kutoka kukosa msimamo wowote hadi kuwa na msimamo wa uhafidina. Siasa, hata hivyo, ilikoma kuwa suala kubwa kwa The Era. Habari zake kuu, ikiwa chini ya Ledger,zilikuwa michezo ,dini ya freemasonna michezo ya kuigiza. Msomaji wa kisasa alisema kuwa, "Katika habari za maigizo ,gazeti hili limezipa nafasi kubwa sana. Katika uhusiano wa kiwango na usahihi wa habari zake za maigizo, gazeti hili ni bora kuliko magazeti mengine ya kila wiki.

Katika tangazo lake moja la 1856, gazeti la The Era lilidai kuwa "Gazeti kubwa kabisa Duniani, likihusisha makala sitini na nne zilizoandikwa katika hati ndogo. Hili ndilo gazeti pekee la kuchapishwa kila wiki linalounganisha faida ya gazeti la michezo na faida ya gazeti la familia. Fasihi, habari za miji na mikoa zimepewa nafasi kubwa sana katika The Era kuliko katika jarida lolote jingine. Maarifa ya Operatic na Muziki, ya nyumbani na ya bara, imekuwa ya kuvutia sana na kuelimisha." The Era likaanza kusemekana kama "Lina thamani sana katika mapitio ya maigizo, habari, uvumi na habari za jumla za maigizo. Pia, ya thamani, ni matangazo mbalimbali ya waigizaji na kampuni."

Mwanahistoria anayejihusisha na maigizo, W. J. MacQueen-Pope, alieleza kuwa The Era kama "Biblia ya Waigizaji" kwa sababu ya habari zake za maigizo zikiwa bora na kuarifu kuliko magazeti mengine:

"Gazeti la The Era lilianza kuandika makala mengi sana kuhusu maigizo(hasa kwa sababu ya matangazo) na masuala ya maigizo huku likichapisha ripoti ya kila wiki kuhusu maigizo ya London na majiji mengine makubwa. The Era likawa jarida muhimu sana la maigizo na kila mtu katika maigizo alilinunua ingawa bei ilikuwa ghali. Ingawaje, kuonekana kama umebeba The Era na kichwa chake kikionekana kwa wapita njia kulionyesha kuwa wewe ndiwe 'mtaalam'. "[1]

The Era liliendelea kuchapishwa mpaka mwanzo wa Vita ya Pili ya Dunia, lakini umaarufu wake na umuhimu wake ulikuwa umedidimia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. The Waterloo Directory of English Newspapers and Periodicals: 1800-1900 at 19th Century British Library Newspapers, Gale Group (requires subscription)
  2. MacQueen Pope, W. The Melodies Linger On, W.H.Allen, 1951, uk. 274-275
  3. The Era katika tovuti ya Arthurlloyd.co.uk