Nenda kwa yaliyomo

Tenapanori

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tenapanori (Tenapanor), inayouzwa kwa jina la chapa Ibsrela, ni dawa inayotumika kutibu ugonjwa wa utumbo unaowashwa na kuvimbiwa choo (IBS-C). [1] Dawa hii inachukuliwa kwa mdomo.[1]

Madhara yake ya kawaida ni pamoja na kuhara, uvimbe wa tumbo na kichwa chepesi.[1] Inaaminika kuwa matumizi yake katika ujauzito na kunyonyesha ni salama.[1] Dawa hii hufanya kazi kwa kuzuia kibadilishaji cha sodiamu-protoni NHE3 ikasababisha kupunguza kunyonywa kwa sodiamu na matumbo.[1]

Tenapanori iliidhinishwa kwa ajili ya matumizi ya kimatibabu nchini Marekani mwaka wa 2019.[1] Kufikia mwaka wa 2021; hata hivyo, ilikuwa bado haipatikani katika maduka ya dawa.[2] Kufikia mwaka wa 2021 ilikwa bado haijaidhinishwa Ulaya wala Uingereza.[3]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 1.5 "Tenapanor Monograph for Professionals". Drugs.com (kwa Kiingereza). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Januari 2021. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Ibsrela Prices and Ibsrela Coupons - GoodRx". GoodRx. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 9 Mei 2024. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Tenapanor". SPS - Specialist Pharmacy Service. 26 Mei 2017. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 25 Septemba 2021.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya tiba bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Tenapanori kama sababu yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.