Tarafa ya Budalangi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tarafa ya Budalangi inapatikana nchini Kenya, kaunti ya Busia.

Budalangi imegawanyika katika divisheni, lokesheni na vitongoji kadha. Ilipandishwa madaraka na kuwa wilaya mnamo mwaka wa 2007 na rais Mwai Kibaki. Kabla ya haya madaraka Budalangi ilikuwa divisheni katika wilaya kubwa ya Busia.

Budalangi yajulikana nchini Kenya kwa sababu ya mafuriko yanayotokea kila mara mwakani. Licha ya sifa duni nchini, imeendelea kiuchumi, kilimo, kisiasa miongoni mwa maendeleo mengi sana. Kilimo kimenawiri Budalangi hasa ukulima wa mpunga unaotegemea maji kutoka kwa mto nzoia.Ukulima huu unaendeshwa na serikali ya kenya kupitia bodi ya unyunyizaji wa mimea. Ukulima unawasaidia wananchi kwa kiwango kikubwa sana kujikimu kwa mahitaji yao ya kila siku. Kuna kilimo cha mimea mingine ikiwemo viazi, mboga, nafaka na kadhalika.