Nenda kwa yaliyomo

Tanna

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tanna (nyekundu) kati ya visiwa vya Vanuatu
Ramani ya Tanna

Tanna ni kisiwa upande wa kusini wa nchi ya visiwa ya Vanuatu katika Bahari ya Pasifiki ya kusini. Ni kisiwa kikuu cha jimbo la Tafea la Vanuatu.

Mji mkubwa ni Lénakel na mji wa Isangel ni makao makuu ya jimbo.

Tanna ina urefu wa kilomita 40 na upana wa kilomita 19 na eneo lake kwa jumla ni km² 550.

Sehemu ya juu zaidi ni mlima Tukosmera wenye kimo cha mita 1,084. Mlima Yasur ni volkeno hai kisiwani.

Jumla ya wakazi ilikuwa watu 28,799 mwaka 2009.

Wakazi wote ni wa asili ya Melanesia na hata kama kisiwa ni kidogo kuna lugha tofauti, zikiwa pamoja na Kitanna-Kaskazini na Kitanna-Kusini-Magharibi.