Sweet Fanta Diallo
“Sweet Fanta Diallo” | |||||
---|---|---|---|---|---|
Jalada la Sweet Fanta Diallo
| |||||
Single ya Alpha Blondy kutoka katika albamu ya Revolution | |||||
Imetolewa | 1987 | ||||
Muundo | (7", Single) | ||||
Imerekodiwa | 1986-1987 | ||||
Aina | Reggae-Pop | ||||
Urefu | 4:45 | ||||
Studio | Pathé Ufaransa | ||||
Mtunzi | Alpha Blondy | ||||
Mwenendo wa single za Alpha Blondy | |||||
|
"Sweet Fanta Diallo" ni jina la wimbo ulioimbwa na kutungwa na mwanamuziki wa miondoko ya reggae kutoka nchini Ivory Coast, Alpha Blondy. Wimbo unatoka katika albamu ya Revolution iliyotoka mwaka 1987.[1][2] Ndani ya wimbo, Alpha alikuwa anasumbuliwa na matatizo ya kisaikolojia na kulazwa katika moja ya hospitali huko nchini Ivory Coast. Alipata tiba na kupona kwa asilimia mia moja. Siku moja alifikiria kurudi pale hospitalini kwa minajili ya kutoa shukrani kwa nesi mrembo sana aliyemsimamia hadi kupona aliyetambulika kwa jina la Fanta Diallo. Matokeo yake ya kwenda kutoa shukrani kwa nesi huyo yaliishia butwaani baada ya kuambiwa ya kwamba hakuna nesi mwenye jina hilo katika hospitali ile. Imani yake iliendelea kumwambia ya kwamba yule alikuwa malaika na si mwanadamu kabisa.[3]
Orodha ya nyimbo
[hariri | hariri chanzo]Kwenye santuri ya wimbo huu kuna nyimbo mbili.
Na. | Jina la wimbo | Albamu |
---|---|---|
1 | Sweet Fanta Dialo | Revolution |
2 | Miri | Revolution |
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Alpha Blondy - Sweet Fanta Diallo". Discogs (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-05-29.
- ↑ "Alpha Blondy And The Solar System - Revolution". Discogs (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2019-05-29.
- ↑ "Reggae Appreciation Society - Abuja". www.facebook.com. Iliwekwa mnamo 2019-05-29.