Nenda kwa yaliyomo

Mlango wa Hormuz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Strait of Hormuz)
Ramani ya Mlango wa Hormuz
Mahali pa Mlango wa Hormuz

Mlango wa Hormuz (Kar. مضيق هرمز - madīq hurmuz, Kiajemi تنگه هرمز - tangeh-ye hormoz) ni mlango wa bahari mwembamba kati ya Uajemi na Falme za Kiarabu unaounganisha Ghuba ya Uajemi na Ghuba ya Omani ambayo ni mkono wa Bahari Hindi.

Upana wake ni kilomita 60 tu. Katikati kuna visiwa vya Abu Musa na Tunbi ambavyo vinakaliwa na jeshi la Uajemi na kudaiwa pia na Falme za Kiarabu.

Marekani yategemea mafuta ambayo hupita humo hivyo huwa na meli za kivita katika mazingira yake. Mwaka 1988 palikuwa na mapigano kati ya manowari za Uajemi na Marekani baada ya Wajemi kufichia mitego ya bahari na kudhurisha meli ya Marekani.