Steve Tilson

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Steve Tilson
Tilson, Steve.jpg
Maelezo binafsi
Jina kamili Stephen Brian Tilson
Tarehe ya kuzaliwa 27 Julai 1966
Mahala pa kuzaliwa    Wickford, Uingereza
Urefu 1.80m
Nafasi anayochezea Mshambulizi / Mchezaji wa kati
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Southend F.C.(meneja)
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
1986–1988
1988–1998
1994
1998–2002
2002–2004
Witham Town
Southend United
→ Brentford (mpango wa mkopo)
Canvey Island
Southend United
Timu alizoongoza
2003- Southend F.C.

* Magoli alioshinda

Stephen Brian "Steve" Tilson (amezaliwa 27 Julai 1966 mjini Wickford,Uingereza) ni meneja wa kandanda nchin Uingereza na ni mchezaji wa kandanda wa zamani. Hivi sasa yeye anasimamia timu ya Southend United, ambayo hucheza katika Ligi ya Uingereza ya Daraja la Pili.

Kazi[hariri | hariri chanzo]

Tilson alianza kazi yake ya uchezaji na timu ya Witham Town ambayo haikushiriki katika ligi kabla ya kuajiriwa na meneja wa South End wa wakati huo,Danny Webb. Katika miaka ya 1990, Tilson alicheza katika mechi takriban 250 na alicheza katika timu iliyoshinda taji la kupandishwa hadi ligi ya daraja la juu. Walishinda hivi mara mbili mfululizo hapo mwanzoni mwa mwongo wa 1990. Tilson alicheza daima katika timu ya Southend, isipokuwa kwa mpango mfupi wa mkopo na timu ya Brentford, mpaka mwaka wa 1998.1998, alitia saini mkataba na klabu ya Canvey Island, akicheza kama nahodha wa klabu katika miaka yake minne katika klabu hiyo.

Katika mwaka wa 2002,Tilson alirejea Southend,wakati huu ili kuongoza kituo chao kipya walichokiita Centre of Excellence. Tilson alifanya kazi katika Southend ili kuendeleza vijana mpaka Steve Wignall alipofutwa kazi katika mwezi wa Novemba 2003. Klabu hiyo ilikuwa imepata hatari ya kushushwa hadi ligi ya daraja lachini,Tilson akaajiriwa kama meneja wa muda mfupi na mwenyekiti Ron Martin.Tilson alichukua jukumu lake na akaendesha klabu kutoka hatarini. Katika msimu uo huo,Tilson aliongoza Southend kuingia fainali yake ya kwanza ya taifa katika historia ya klabu huku wakishindwa 2-0 na Blackpool katika fainali ya Football League Trophy. Katika mwezi wa Machi 2004,Tilson alipewa kazi ya kuwa meneja kamili wa timu hiyo na akakubali.

Katika misimu miwili ilyofuata,Tilson aliendesha Southend kupandishwa mara mbili kutoka Ligi ya League Two hadi kuingia Ligi ya Championship. Southend,pia, ilifika fainali nyingine ya Football League Trophy katika mwaka wa 2005 lakini wakshindwa na Wrexham. Mafanikio ya Tilson yalimfanya ahusishwe na kazi katika timu za West Bromwich Albion na Norwich City lakini akaendelea kufanya umeneja wake katika timu ya Southend. Mnamo Novemba 2006, Southend ilipta mafanikio yasiyosahauliwa hasa ushindi dhidi ya mabingwa wa Ligi Kuu,Manchester United katika Shindano la Kombe la League,lakini wakashushwa kutoka ligi ya Championship katika msimu huo.

Tarehe 3 Januari 2009, Tilson aliongoza Southend katika mechi iliyotoka 1-1 katika Shindano la Kombe la FA dhidi ya timu ya Chelsea. Peter Clarke akifunga bao la kusawazisha katika dakika za mwisho ya mechi. Mnamo 28 Oktoba 2009,kufuatia klabu kuwa kutishiwa na utawala na mchezaji Lee Sawyer kurudi Chelsea,Tilson alirudi kuchezea klabu ya Southend katika shindano la Kombe la Assex.

Takwimu ya Usimamizi[hariri | hariri chanzo]

Sahihi kama ilivyo 1 Novemba 2009

Klabu Uzalendo Tangu Hadi Matokeo
G W L D Mechi Alizoshinda %
Southend United Uingereza 20 Novemba 2003 Sasa 326 137 109 80 42.02

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. ^. BBC Sport. 2004-03-11. "Southend appoint Tilson"
  2. ^ . BBC Sport. 2006-11-08. "Tilson revels in Southend cup win"
  3. ^ 2009-10-28. "Blues exit Senior cup". Southend United.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]