Nenda kwa yaliyomo

Stamata Revithi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Stamata Revithi (1866 – baada ya 1896) alikuwa mwanamke wa Kigiriki aliyekimbia marathon ya kilomita 40 wakati wa Michezo ya Olimpiki ya Majira ya Joto ya 1896. Michezo hiyo haikuruhusu wanawake kushiriki, lakini Revithi alisisitiza kwamba aachiliwe akimbie. Revithi alikimbia siku moja baada ya wanaume kumaliza mbio rasmi, na ingawa alikamilisha marathon kwa takriban saa 5 na dakika 30 na kupata mashahidi waliotiwa saini kuthibitisha muda wa mbio, hakuruhusiwa kuingia Uwanja wa Panathinaiko mwishoni mwa mbio. Alikusudia kuwasilisha nyaraka zake kwa Kamati ya Olimpiki ya Kigiriki kwa matumaini kwamba wangethibitisha mafanikio yake, lakini haijulikani kama alifanya hivyo. Hakuna rekodi inayojulikana ya maisha ya Revithi baada ya mbio yake.[1]

Kulingana na vyanzo vya wakati huo, mwanamke wa pili, "Melpomene", pia alikimbia mbio ya marathon ya 1896. Kuna mjadala miongoni mwa wanahistoria wa Olimpiki kama Revithi na Melpomene walikuwa mtu mmoja au la.[2]

  1. Olympic historians do not all agree on why Revithi decided to run the marathon race. It is thought by some of them that Revithi's goal in this decision was to secure a position for work (DeFrantz, Women in Sport, 185; Eleftheratos, 11 April 1896 [PDF]). Jere Longman (In Footsteps of History) wonders "why anyone would want to run 24 miles for a civil service job". According to Martin & Gynn (Running through the Ages, 21), "the male runner told her (Revithi), apparently in jest, that the best way to get rich was to run the marathon and win" (see a similar version of the story by Tarasouleas [The Female Spiridon Loues, 11; Stamata Revithi, "Alias Melpomeni", 53]). Emet Malone (And at the Starting Line... Archived 2018-09-19 at the Wayback Machine) believes that, after Revithi was rejected, "she ran the course anyway to prove a point".
  2. Tarasouleas, Stamata Revithi, "Alias Melpomeni", 53; Tarasouleas, The Female Spiridon Loues, 11
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Stamata Revithi kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.