Shirikisho la Mpira wa Kikapu la Angola
Angolan Basketball Federation Ni bodi inayoongoza na mashindano rasmi ya mpira wa vikapu nchini Angola. FAB ilianzishwa mwaka 1976, na Bw. José Jaime de Castro Guimarães akihudumu kama mwenyekiti. mwanzoni Shirikisho hilo lilikuwa Rua Rainha Ginga na baadaye kuhamishiwa kwenye ghorofa ya chini ya jengo lililo katika Kiwanja cha Michezo cha Cidadela.
FAB inasimamia shughuli za vyama 18 vya mpira wa kikapu nchini.Kwa kawaida shirikisho hilo lina watumishi 42, wakiwemo wajumbe 3 wa mkutano mkuu, 3 wa kamati ya ukaguzi, 5 kutoka bodi ya sheria, 5 kutoka bodi ya nidhamu na washiriki 16 huku menejimenti ikiwa na wajumbe 10.
Kwa msingi wa kila mwaka, shirikisho hilo huandaa michuano ya kitaifa ya wanaume iitwayo BAI Basket, ubingwa wa wanawake pamoja na Angolan Cup na Super Cup, ikijumuisha katika kategoria za vijana walio chini ya umri.Pia inasimamia michuano ya majimbo inayoandaliwa na vyama vinavyohusiana na mpira wa vikapu na ushiriki wa vikosi vya kitaifa katika matukio ya Afrika na duniani kote.